Uchaguzi 2020 Rais, sisi watumishi tatizo letu kubwa na CCM ni kutopata nyongeza ya mishahara kwa muda mrefu

kzba

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Posts
1,355
Reaction score
789
Pamoja na maono na fikra zako za kuamini kuwa sisi watumishi kura zetu ni chache na hazitakusaidia chochote kwenye ushindi wako, ila ni ukweli usiopingika kuwa sisi watumishi tuna ushawishi mkubwa wa kuhamasisha watu wakupigie kura kuliko huyo unaemuamini Polepole au Bashiru na hao walinzi wako.

Suala la maslahi ni zito na halivumiliki kuliko hayo mengine yanayosemwa na wapinzani wako ambayo naamini kabisa ukipata washahuri wazuri unaweza kuyabadilisha muda wowote, naamini hata wewe mwenyewe mtu akiingilia maslahi yako hautomuacha salama.

Kingine nikukumbushe tu Rais, hizi pesa za watumishi kuongezewa mishahara hazitatoka kwenye mfuko wako mkuu wa serikali, kila taasisi ilishaweka bajeti ya kupandisha mishahara watumishi wake tangia 2016 na hizo pesa zipo mpaka sasa ila walikuwa wanasubiri tamko lako tu watumishi waweze kupandishiwa mishahara hiyo.

Mh rais, una muda mchache wa takribani siku 33 kuzikomba kura za watumishi hawa kama nilivyokushahuri hapo juu, wewe bado ni rais, kama umeweza kutoa matamko mbalimbali katika mikutano yako ya kampeni kama vile barabara kujengwa katika kipindi cha kampeni hizi basi naamini hata hilo unaweza kulitolea tamko popote ndani yani ya siku hizi chache zilizobaki na ukavuna maelfu ya kura zetu.

Naamini ukifanya hivyo hata wapinzani wako watakosa hoja lakini vinginevyo utaicha ikulu kwa fedhea kwa wapinzani wako Mh. rais, ni ushahuri tu.

"No hate no fear, CCM mbele kwa mbele, ubwabwani, kazi na bata"
 
Kwa wafanyakazi, chini ya Magufuli:- mishahara haitopanda, mkiacha/achishwa/maliza mikataba ikiisha, hamtopewa mafao, mkistaafu mtakumbana na kikokotoo kinacho toa mafao kiduchu!. Huyu jamaa hayupo kwa ustawi wa watu hilo mlijuwe na liwakae vichwani mwenu.
 
Basi kama ni hivyo lile jambo letu oct 28 litatimia na tusilaumiane kwa maamuzi yetu magumu sisi watumishi.
 
Pamoja na maono na fikra zako za kuamini kuwa sisi watumishi kura zetu ni chache na hazitakusaidia chochote kwenye ushindi wako, ila ni ukweli usiopingika kuwa sisi watumishi tuna ushawishi mkubwa wa kuhamasisha watu wakupigie kura kuliko huyo unaemuamini Polepole au Bashiru na hao walinzi wako.

Suala la maslahi ni zito na halivumiliki kuliko hayo mengine yanayosemwa na wapinzani wako ambayo naamini kabisa ukipata washahuri wazuri unaweza kuyabadilisha muda wowote, naamini hata wewe mwenyewe mtu akiingilia maslahi yako hautomuacha salama.

Kingine nikukumbushe tu Rais, hizi pesa za watumishi kuongezewa mishahara hazitatoka kwenye mfuko wako mkuu wa serikali, kila taasisi ilishaweka bajeti ya kupandisha mishahara watumishi wake tangia 2016 na hizo pesa zipo mpaka sasa ila walikuwa wanasubiri tamko lako tu watumishi waweze kupandishiwa mishahara hiyo.

Mh rais, una muda mchache wa takribani siku 33 kuzikomba kura za watumishi hawa kama nilivyokushahuri hapo juu, wewe bado ni rais, kama umeweza kutoa matamko mbalimbali katika mikutano yako ya kampeni kama vile barabara kujengwa katika kipindi cha kampeni hizi basi naamini hata hilo unaweza kulitolea tamko popote ndani yani ya siku hizi chache zilizobaki na ukavuna maelfu ya kura zetu.

Naamini ukifanya hivyo hata wapinzani wako watakosa hoja lakini vinginevyo utaicha ikulu kwa fedhea kwa wapinzani wako Mh. rais, ni ushahuri tu.

"No hate no fear, CCM mbele kwa mbele, ubwabwani, kazi na bata"
Kikokotoo na fao la kujitoa linawahusu pia.
 
Back
Top Bottom