Rais TFF atuma salamu za pole kwa wahanga wa mafuriko

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,229
Reaction score
610
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salaam za pole kwa wakazi wa Dar es salaam na hasa wale walioathirika na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam kwa siku ya tatu mfululizo sasa.

Katika salam zake kupitia kwa Mkuu wa Mkoa Dar es salaam, Mecky Sadik, Malinzi amesema familia zimepoteza makazi, miundombinu ya usafiri na michezo imeharibika na hata kuwa katika hali ya kutotumika, wanawake watoto, familia, shughuli za kiuchumi na kimichezo zimeathirika na mvua hizi.

TFF inaunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa Dar es salaam, Serikali na wadau wote wanaoshugulika kupunguza makali ya janga hili.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Mei 8, 2015.
 
Salamu hizo ni kejeli kwa Yanga, maana nao ni waathirika wa hizi mvua...
 
Hivi wadau huyu Rais wa TFF kila kukicha ni salamu na kushinda mitandaoni mie namuona bomu bora hata Ndolanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…