Wakuu nimekutana na hii video ikisambaa katika mitandao ya kijamii na kuelezwa kuw Rais Wa Marekani Donald Trump amezidiwa na amekimbizwa hospital
Your browser is not able to display this video.
Tunachokijua
Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na kipande cha video kinachoonesha msafari wa magari ukiwa na ving'ora na kusababisha magari mengine kusimamam na kuelezwa kuwa ni msafara wa Rais Donald Trump akiwahishwa hospital.
Chanzo kimoja kiliandika.
"Taarifa zisizothibitishwa zinaeleza Rais Trump amekimbizwa hospital, barabara zafungwa"
Uhalisia wa madai hayo
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia nyenzo za kidigitali umebaini kuwa taarifa hizo si za kweli.
Ufuatiliaji kwa kutumia maneno muhimu umejirirdhisha kuwa hakuna chanzo chcohote cha kuaminika ndani na nje ya Marekani kilichochapisha hiyo kueleza kuwa Rais Trump amekimbizwa hospital.
Aidha video iliyoambatanishwa na Taarifa hizo si ya mwaka 2026, video hiyo ilichapishwa mwaka 2024 wakati Rais Donald trump aliposhambuliwa kwa risasi alipokuwa akifanya kampeni za kugombea Urais.
Hata hivyo hakuna Taarifa yyote kutoka Ikulu ya Marekani ama Donald Trump mwenyewe kuthbitisha kuwa hali ya kiongozi huyo ni mbaya na hivyo amekimbizwa hospitalini.
Vile vile Ras Trump ameonekana akiendelea kuchapisha taarifa mbalimbali kupitia ukurasa wake wa Truth kuelezea mambo mbalimbali ikiwemo vita inayoendelea baina ya na Iran na wao.