MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Kwa mujibu wa matokeo yanayotiririka kutokea maeneo mbali mbali ya nchi, tarakimu zinaonyesha rais Uhuru ametimiza 7,263,496, idadi hii imebakia kidogo tu kufikia milioni nane alizokua nazo kwenye uchaguzi wa mwanzo.
Japo pia inaeleweka changamoto za kutotimiza ni kwamba
- Kwenye kinyang'anyriro maalum cha mwanzo, maelfu ya Wakenya walisafiri kwenda vijijni kupiga kura, lakini ni wachache walisafiri kwenye zoezi hili la marudio.
- Kuna wengi pia hawakua na hamasa ya kujitokeza kupiga kura kwa kauli kwamba mshindani alikua mmoja, hawakuona haja ya kuhangaika kwenye mafoleni.
- Maeneo yenye wafuasi wa Raila yalishuhudia uhuni wa kila aina. Vijana walifunga kabisa gatuzi nne zenye wapiga kura zaidi ya milioni
- Pia kuna maeneo kama Bungoma ambapo waliopiga kura waliamka na kukuta nyumba zao zimetiwa alama ya rangi nyekundu kama ishara kwamba wajiandae kwa mtiti ujao
Lakini pia pamoja na yote hayo, wafuasi wa Raila nje ya Nyanza walisusia kabisa na hawakupiga kura, hivyo nchi imegawanyika. Juzi Raila ameagiza wakae mkao wa mapambano na kwamba wasusie huduma zote za makampuni yenye ushirikiano wa aina yoyote na serikali.
Kwa kifupi, mapambano haya ya siasa hayataisha hivi karibuni, wananchi wa chini kama kule Kibera wajiandae kwa hali na mali maana kuna mikimbio ya kila siku hadi mmoja wa hawa mafahali wawili atakapochoka na kuiachia nchi iendelee mbele.
Kenya Elections 2017 - Daily Nation