Rais Uhuru Kenyatta apunguza bei ya mafuta kitoka 16% hadi 8%

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Wananchi wengi wameelezea furaha yao kufuatia hatua ya Rais Kenyatta kuchukua uamuzi mgumu kwa kukubali kupunguza bei ya bidhaa ya mafuta kutoka 16% hadi 8%.

Katika hotuba kwa taifa hapo jana Rais Uhuru Kenyata amesema kuwa amesikia kilio cha Wakenya kuhusu kupanda kwa bei za bidhaa mahitajio na usafiri.

Mbali na kupunguza kodi ya mafuta, Rais Kenyatta amepinguza gharama za mapokezi , burudani, mafunzo na mikutano, na usafiri katika nchi za nje.

Hata hivyo amependekeza kuongezwa fedha katika idara za utekelezaji wa sheria na hivyo kuweza kukusanya kipato zaidi kupitia mahakama nchini ambapo mapendekezo yote hayo
yanasubiri kuidhinishwa bungeni wakati wa kikao maalum Septemba 18 mwaka huu.

Hata hivyo bado serikali ya Kenya ina kazi kubwa ya kulishawishi Shirika la Fedha Dunia IMF na kujua wapi itakapopata zaidi ya dola milioni 90 kuziba pengo katika nakisi ya bajeti.

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la kuorodhesha uwezo wa mataifa kukopa, Kenya inakabiliwa na ongezeko la deni la taifa ambalo kwa sasa linakadiriwa kuwa limefika 58% ya pato jumla la nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…