Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Muswada huu ni miongoni wa miswada mingine 9 ambayo Rais Uhuru Kenyatta ametia saini kuwa sheria juma hili.
Miswada mingine ni pamoja na ile ya mkaguzi wa hesabu za Serikali, muswada wa fedha za matumizi ya ziada, muswada wa baraza la taifa la mitihani, muswada wa haki ya ardhi asilia, muswada wa haki za kueleza tamaduni,muswada wa utunzaji wa misitu, muswada wa sheria ya sheria ya ardhi na ule wa bidhaa za kilimo.
Kipengele cha sheria ya haki ya kupata taarifa, kifungu namba 35 cha katiba ya Kenya, kinaipa mamlaka tume ya mahakama na bodi maalum iliyoundwa kuhakikisha utekelezaji wa sheria hiyo mpya.
Sheria hii mpya sasa unaondoa ukiritimba ulikuwepo awali kutoka taasisi fulani za serikali ambazo zilikuwa zinasifika kwa kuwanyima wananchi taarifa kwa kile ofisi hizo zilikuwa zikidai ni siri.
Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Transparency, linasema sheria ya haki ya kupata taarifa ni suala la lazima kwa ofisi za umma kutoa taarifa kuhusu serikali na taasisi zake, kuhusu inachofanya, wafanyakazi wake na muundo wa mishahara.
Sheria hii pia inalazimika taasisi nyingine za serikali kuelezea kwa umma hatua ambazo imechukua, sera au maamuzi kwa wananchi wake ikiwa watataka kufahamu.