sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,745
- 1,171
Uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani nchini Tanzania kwa mwaka 2020,huenda ukawa uchaguzi bora kuliko yote au uchafuzi kuliko yote toka tuingie chaguzi chini ya mfumo wa vyama vingi 1995.
Ubora au udhaifu wa uchaguzi huu unajengwa na kauli za mtukufu rais ambaye ndiye mwenye mamlaka ya uteuzi ambao kupitia kwayo, wateuliwa msimamizi mkuu na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ndiyo tulio nao leo na ufanisi wao umeshaanza kuleta athari kwa kusababisha rufaa zaidi ya 500.
Kwa kuwa Rais huyu ndiye amiri jeshi mkuu wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama, ambaye kupitia mamlaka yake ya uteuzi amemteuwa IGP Sirro, anayefanya kazi ya tume ya uchaguzi kwa kuwatisha wadau wa uchaguzi ambao ni wananchi chini ya itikadi yao inayo tofautiana na mamlaka ya uteuzi,ameshindwa kumkemea kwa kauli zake za kiuchochezi zenye lengo la kuibeba CCM . Kwa mwenendo huu ,msemo wa wahenga kuwa fisi akiwa hakimu mbuzi hana haki!!!! unakosaje kuaminiwa.
Katika asili ya uumbaji, maandiko yanatuasa kuheshimu na kutii mamlaka ya sheria, ambayo inamtabanaisha rais na mamlaka yake.
Lakini amri hii ya kimungu inajengwa na msingi mkubwa wa uadilifu kwa waliokuwa viongozi wa umma, sidhani utii huu wa sheria leo unaweza kuandikwa kwa kizazi hiki ambacho hakiheshimu mamlaka ya sheria kuanzia wasimamizi wenyewe wa sheria.
Na hapo ndipo viongozi wetu wa dini wanapoingizwa mkenge na watawala kuitukuza batili kwa kuikandamiza haki kwa kulinda mirija tumbo isikatwe kwa kulazimisha kutii mamlaka bila kukemea maovu yanayo sababisha wananchi wasitii mamlaka hizo, hapo ndipo tofauti ya watawala wa dini na viongozi wa dini inapo jiinua.
Viongozi wa dini ambao ndiyo viongozi wa kiroho hufungwa kwa vifungo vya imani kwa kuichukia dhambi na kumtukuza Mungu kwa kuimarisha haki, haki ambayo tunaambiwa ndilo tunda la amani kwa kuwa Haki huinua taifa,wameacha majukumu yao wamekubali kuwa mashereheshaji kwa watesi wetu.
Tukiangalia historia ya mfumo wa vyama vingi nchini utaona kuwa Watanzania/Watanganyika si wageni wa mfumo wa vyama vingi, waliuishi kabla ya uhuru na leo baada ya uhuru l. Baada ya kuujaribu mfumo wa chama kimoja ulihodhi mamlaka ya umma na kuimarisha ulafi wa madaraka ambao hautofautiani na unyani (APE DO MIA) na kuamua kurudi kwenye mfumo walio uzoea kabla ya Uhuru #MULT PART SYSYEM.
Mfumo guy ulioridhiwa kisheria baada ya kuheshimu maoni na maridhiano ya wananchi.
Ndiyo maana bunge letu kupitia ushawishi wa Mwalimu kwenye NEC liliupitisha rasmi kuwa Tanzania ni nchi ya mfumo wa vyama vingi.
Lakini pamoja na kupitishwa kisheria, bado ulevi wa madaraka wa kimfumo uliendelea kukiathiria chama chao kwa kuwa ulishinikizwa zaidi na Mwalimu Nyerere kuliko chama chenyewe kwa hofu ya kupoteza madaraka yao.
Na Kwa kuwa mfumo huo wa chama kimoja ulihodhi mamlaka na kulewa madaraka ndipo dhana ya chama kushika hatamu ilipo walewesha watawala wa nyakati zile na kushindwa kuutokomeza ndani ya CCM ya leo .
Hali iliyo pelekea kushindwa kuweka mifumo ya kisheria itakayo ondoa dhana nzima ya ubinafsi iliyo tawala ndani ya CCM kuwa ndicho chama chenye haki ya kutawala kuliko vyama vingine.
Hata Rais Magufuli akihutubia Taifa mbele ya Mabalozi wa nchi za nje nchini Tanzania, aliahidi uchaguzi huru na haki Hali akijuwa anapingana na dhamira yake na matakwa ya chama chake.
Pia hakuzingatia kuwa nyuma ya hotuba yake kuna maamuzi ya mahakama kuu kutowatambua makada wa CCM kwa nyadhifa za Wakurugenzi kusimamia uchaguzi mkuu.
Hakuzingatia kuwa hotuba yake ilipingana na msimamo wake na chama chake kwa kuwa hakuna kanusho lolote kupinga agizo la Rais kwa wasimamizi wa uchaguzi iwapo watawatangaza Watanzania waliopewa nembo ya #WAPINZANI hatowaelewa, kwa kuwa nyadhifa zao wamezipata kutokana na serikali ya CCM.
Kwa kuzingatia yaliyo tajwa hapo juu utaona jinsi gani hayo matukio yanavyohii aondoa dhana nzima ya uchaguzi wa kidemokrasia utakao kuwa wa haki na huru. Ndiyo maana tuna sikia matamko ya vitisho toka vyombo vya dola kwa kujua hotuba ya Rais kwa mabalozi(mabeberu) haihusiani na rangi halisi na matakwa ya CCM.
Hizo ndizo baadhi ya kasoro au viashiria vya uchaguzi kutokuwa wa haki na huru.
Kwa imani ya Rais aliyo ijenga kwa mabalozi kuhusiana na uchaguzi, itakuwa na tija sana ikiwa Tume hiyo aliyo iteua itakuwa ni Tume ya umma si ya Watawala kwa matakwa ya mamlaka ya uteuzi,kwa kuacha vigisu kwa vyama mbadala na kukibeba CCM kwa matakwa ya hisani, yaani mtumikie kafiri upate mradi wako.
Viashiria vya mbeleko kwa CCM kwa misingi ya kukanyaga haki kwa kuviburuza vyama mbadala kwa kuzingatia tamko la Rais/mwenyekiti kwa wakurugenzi kutowatangaza Wapinzani vinaitia doa Tume ya Uchaguzi na kuifanya kuwa Tume ya mkakati wa uchaguzi dhidi ya WAPINZANI.
Uthibitisho mbali na kuwaengua wapinzani hata rufaa zao zinacheleweshwa bila Maelezo ya kina, hali inayoweza kuzua tafrani kwa wananchi wenye jukumu la kuisimika serikali.
Ni vizuri Tume kuacha ukaidi kwa kibri cha mamlaka ya uteuzi, kwa kuwa uhuni hauvumiliki unaweza kusababisha uvunjifu wa uvumilivu kwa wananchi na kuzua sintofahamu.
Mhe. Rais, CCM ilisajiriwa kwa mujibu wa sheria kuwa chama cha siasa ideology yenu ujamaa na kujitegemea, kirudisheni kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi kwa kuacha kuwa tegemezi na kukifanya kuwa chama - dola. Tushawishi kwanini tukuchague tena bila vitisho.