Rais usiusahau Mwenge wa Uhuru

Rais usiusahau Mwenge wa Uhuru

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Mh. Rais Samia wiki mbili hivi zimepita ulitamka kuwa umetuma kikosi kazi kutathmini hali ya mashirika ya Umma ili kupata jibu lipi lifutwe, lipi libinafsishwe na lipi liboreshwe. Good.

Ni kweli tumekuwa na mashirika ya Umma ambayo ni kichaka cha uhujumu uchumi, hayana tija. Na kuna mashirika au taasisi za Umma majukumu yake yanaweza kufanywa na mashirika mengine.

Mimi ombi langu ni huu MWENGE WA UHURU, huu mwenge umekuwa taasisi kamili. Upelekwe makumbusho tu inatosha sasa.

Ikilazimika sana mkauwashe hukohuko na kuuzima hukohuko. Mitaani usionekane anayetaka akauchungulie makumbusho.

Au ufutwe kabisa. UHURU tushaupata sasa watu wapate uhuru wa kiuchumi.

Tanzania bado watu wanalala chumba kimoja na kuku, mbuzi na bata. Huo sio uhuru.

Tanzania kuna watoto wana viribatumbo, hawana chakula bora na cha kutosha. Huo sio uhuru.

Mpaka leo hii wenye vyeti vya form four hata milioni 10 hawafiki, huo sio uhuru.

thumb_1600_800x420_0_0_auto.jpeg
 
Hujui, mwombe Mheshimiwa awape Waarabu huo mwenge.
 
Kwenye Mwenge naungana nawe, IFIKE PAHALA UZIMWE SASA UWEKWE MAKUMBUSHO YA TAIFA.

Mwenge umekua chanzo cha Maambukizi ya Magonjwa ya zinaa sehemu utakapolala, wanaokesha na mwenge hungonoka usiku kucha na asubuhi ni mabaki ya condoms ya kutosha hukutwa.


Mwenge umepoteza maana halisi ile iliyokuwepo enzi za Mwalimu na Uhuru wa Tanganyika.

Uzimwe sasa, Uzimwe.
 
KUNA MUDA NAOMBEA HUO MWENGE UIBWE NA MAJAMBAZI

NAWEZA NKASHEREHEKEA MWEZI MZIMA MIMI NA FAMILIA YANGU
 
Mwenge ni tambiko moja hatari sana, hauwezi kufutwa
 
Mwenge kwangu Mimi hauna tatizo kama kweli kuna sababu za kutosha ili kuuenzi basi ziendelee.

Lakini baadhi ya wananchi wanachukia Mwenge kwasababu zifuatazo:-
1.Kueneza Magonjwa ya kuambukiza ikiwemo HIV
2.Michango ya Lazima
3.Wakimbiza Mwenge kutweza viongozi mbalimbali na kuwaweka mahabusu.
4.Wakimbiza Mwenge kufungashiwa Zawadi zenye harufu ya Rushwa
5.Magari/mafuta ya taasisi kutumika hovyo na kuharibika
6.Huduma muhimu kusimama kutokana na watendaji kutoa kipau mbele kwa mwenge zaidi ya wiki.
7. Ajali
 
Back
Top Bottom