Rais wa Afrika kuongoza FIFA kwa muda

Lumbi9

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2014
Posts
8,666
Reaction score
12,178
Kiongozi wa shirikisho la soka barani Afrika Issa Hayatou kutoka Cameroon amepewa jukumu la kuongoza shirikisho la soka duniani Fifa kwa muda.

Hayatou atachukua usukani kufuatia kusimamishwa kazi kwa Rais wa Fifa Sepp Blatter kwa muda wa siku 90 na Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo, shirikisho hilo linalosimamia soka duniani limesema kupitia taarifa.

Hayatou, aliyeongoza CAF tangu 1988, atachukua usukani kwa mujibu wa sharia za Fifa, akiwa ndiye makamu wa rais katika kamati tendaji ya Fifa aliyehudumu muda mrefu zaidi.

Chanzo: BBC
 

Attachments

  • 141103144226_issa_hayatou_caf_512x288_afp.jpg
    7.5 KB · Views: 221


Congratulation to Issa Hayatou despite that the guy is the Sepp Blatter of Africa - CAF
 
Mbona huyu naye mpigaji tu, imekuwaje kapewa hilo shavu...
 
Naona Michel Platin pia amesimamishwa kwa muda alafu Platin yuko against Blatter.
 
sasa naanza kuamini kweli huu ni mwaka wa mabadiliko.
 
Hongera zake,ila na yeye asipige mahela kwa siku hizi 90,maana Platin kasimamishwa kwa kupokea Euro milioni 4,mwaka 2001.na mwaka 2011.FIFA kuna Escrow pia
 
Mbona huyu naye mpigaji tu, imekuwaje kapewa hilo shavu...

Huyu naye ni shida tu!! lazima atapiga tu kwani huyu naye CAF, ameshaifanya kama yake!! kama alivyokuwa blatter ameifanya FIFA, kweli mwisho wa ubaya ni aibu huyu mzee alijifanya kuwa bila yeye hakuna fifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…