Rais wa Angola, JoΓ£o LourenΓ§o ahitimisha ziara ya Kitaifa, aondoka nchini

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
π—₯π—”π—œπ—¦ 𝗝𝗒Ã𝗒 π—Ÿπ—’π—¨π—₯π—˜π—‘Γ‡π—’ π—ͺ𝗔 π—”π—‘π—šπ—’π—Ÿπ—” π—”π—›π—œπ—§π—œπ— π—œπ—¦π—›π—” π—­π—œπ—”π—₯𝗔 𝗬𝗔 π—žπ—œπ—§π—”π—œπ—™π—”, π—”π—’π—‘π——π—’π—žπ—” π—‘π—–π—›π—œπ—‘π—œ

Rais wa Jamhuri ya Angola, Mhe. JoΓ£o Manuel GonΓ§alves LourenΓ§o, amehitimisha ziara yake ya kitaifa ya siku tatu nchini na kuondoka kurejea nchini Angola, Oktoba 30, 2026.

Katika ziara hiyo, Rais LourenΓ§o alifanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kupanua ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo kati ya mataifa hayo mawili.

Akiwa jijini Dodoma, Rais LourenΓ§o alishiriki hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba pamoja na miundombinu ya barabara zake.

Mheshimiwa LourenΓ§o aliagwa rasmi na mwenyeji wake Rais Samia katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma kabla ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Dodoma.

Katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma Mheshimiwa LourenΓ§o alisindikizwa na kuagwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb.) Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Balozi wa Tanzania anayewakilisha Angola mwenye makazi yake Zambia Injinia Cyprian Luhemeja, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Angola Bw. Mbwana Mziray na viongozi wengine wa Serikali.
 

Attachments

  • IMG-20261031-WA0021.jpg
    253.6 KB · Views: 2
  • IMG-20261031-WA0027.jpg
    411.1 KB · Views: 2
  • IMG-20261031-WA0035.jpg
    450.2 KB · Views: 2
  • IMG-20261031-WA0043.jpg
    356.8 KB · Views: 2
  • IMG-20261031-WA0037.jpg
    673.3 KB · Views: 2
  • IMG-20261031-WA0039.jpg
    400.4 KB · Views: 2
  • IMG-20261031-WA0041.jpg
    472.8 KB · Views: 2
  • IMG-20261031-WA0033.jpg
    438 KB · Views: 2
  • IMG-20261031-WA0031.jpg
    265.7 KB · Views: 2
  • IMG-20261031-WA0029.jpg
    374.3 KB · Views: 2
  • IMG-20261031-WA0023.jpg
    366.8 KB · Views: 2
  • IMG-20261031-WA0025.jpg
    666.1 KB · Views: 2
  • IMG-20261031-WA0019.jpg
    512.3 KB · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…