Rais wa Barcelona atoa tamko

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299


Rais wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu amewaomba wachezaji wa Barcelona, mashabiki na makocha kushikamana pamoja baada ya kufungwa na AS Roma na kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa jana usiku.


"Kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa ni mshituko mkali sana kwa mashabiki wote wa Barcelona, lakini sasa ni wakati wa mashabiki, makocha na wachezaji kuwa na umoja zaidi kuliko hapo awali,'' ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.


Barcelona ambayo kwa msimu wa pili mfululizo imeendolewa kwenye robo fainali na klabu za Italia baada ya msimu uliopita kutolewa na Juventus, jana usiku ilikubali kichapo cha mabao 3-0 hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa 4-4 huku Roma ikiwa na faida ya bao la ugenini kutokana na kupoteza 4-1 nchini Hispania.

Barcelona sasa imefikisha misimu mitatu mfululizo ikitolewa katika hatua ya robo fainali huku wapinzani wao Real Madrid wakiwa wanafukuzia ubingwa wa Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo. Ilitolewa na Atletico 2016, Juventus 2017 sasa Roma.


Kiungo mkongwe wa Barcelona Sergio Busquet amesema matokeo hayo yamewaumiza timu nzima kutokana na mipango waliyokuwa wamejiwekea ya kutwaa taji hilo baada ya muda mrefu kupita.


Chanzo: EATV
 
walizoea kubwa kwa kuanza ugeunini na kumalizia nyumbani sasa wameanzia nyumbani wakafa ugenini
 
Roma haijajengwa kwa siku moja na inaelekea bado Roma ipo kwenye mihangaiko ya kuendelea kujengwa

So jana akina Dzeko walikuwa wanaendelea na ujenzi wa Roma just a [emoji189] [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Barca akacheze la liga tu. Mimi ningeumia sana kama Roma angetolewa, maama mchezo wa kwanza walikufa kiume, tena baada ya kufanya makosa madogomadogo yanayoepukika kabisa. Messi anaendelea kujidhihirisha kuwa si chochote nje ya la liga
 
Barca ya sasa ni ya kawaida tu kama team zingine za kawaida inaweza kufungwa na team yoyote tu.
Kwani ukimtoa Messi na Suarez nani mwingine humo ni talented player ?
 
Barca ilikuwa ya kina Etoo,Ronaldinho,Kluivert bwana.Kina Iniesta washazeeka sasa.Nakumbuka île Barça ya mwaka 2006 iliyowafunga Arsenal pale Stade de France jijini Paris.
 
Barca ilikuwa ya kina Etoo,Ronaldinho,Kluivert bwana.Kina Iniesta washazeeka sasa.Nakumbuka île Barça ya mwaka 2006 iliyowafunga Arsenal pale Stade de France jijini Paris.
ilikuwa kabla ya werld cup 2006 ujerumani iyo. Ronaldihno alikuwa ndio kavuma hasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…