SI KWELI Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye anusurika kupinduliwa akitoka kwenye mkutano wa UNGA 2023

SI KWELI Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye anusurika kupinduliwa akitoka kwenye mkutano wa UNGA 2023

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Hii habari ya rais wa Burundi kutaka kupinduliwa nimeiona Twitter!! baada ya speech yake alivotoka UN.

IMG_9618.jpg

Je ina ukweli wowote?
 
Tunachokijua
Mjadala Mkuu wa kikao cha sabini na nane cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (United Nations General Assembly-UNGA) ulifunguliwa Septemba 19 na uliendelea hadi Septemba 26, 2023 ambapo viongozi mbalimbali kutoka nchi kadhaa wanachama walihutubia mkutano huo.

Mkutano huo kwa mara ya kwanza ulifanyika Januari 10, 1946, London, Uingereza ambapo nchi wanachama 51 walihudhuria.

Kwa sasa, mkutano huu hupata uwakilishi wa nchi 193 na pamoja na mambo mengine huangazia masuala ya kimataifa ikiwemo yale yanayohusu ulinzi na amani.

Kuibuka kwa madai ya jaribio la Mapinduzi
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye alikuwa ni miongoni mwa washiriki wa mkutano huo ambao kwa mujibu wa ratiba, alihutubia asubuhi ya Septemba 21, 2023.

Baada ya mkutano huo, taarifa za jaribio la kupinduliwa kwa Rais huyu zilianza kusambaa. Mathalani, Oktoba 2, 2023 kupitia mtandao wa X, akaunti inayoitwa The Chronicles ilitoa taarifa kuwa Rais Ndayishimiye alidokeza kuwa wakati anatoka mkutanoni, wasaidizi wake walimtaka asafiri kwa ndege hadi Tanzania, kisha aingie Burundi kwa njia ya barabara ili kukwepa mapinduzi.

Pia, taarifa hiyo ilisema kuwa pamoja na majaribio mengi ya mapinduzi yanayofanyika, yeye alikuwa hana hofu na kwamba Mungu alikuwa anamlinda.

Pamoja na kusambaa sana kwa taarifa za jaribio la mapinduzi haya, bado chanzo chake halisi hakijafahamika.

Baada ya kurejea Burundi, Jumapili ya Oktoba 1, 2023, Rais Ndayishimiye aliyatupilia mbali madai hayo yenye uzushi aliyosema yalikuwa yanatolewa na watu wasioitakia mema Burundi, ambao walikuwa na lengo ovu la kuleta picha mbaya kwa nchi hiyo.

1911bda7b952473bbf94ccd6653bb6ea_18.jpeg

Evariste Ndayishimiye, Rais wa Jamhuri ya watu wa Burundi
Aidha, Rais Ndayishimiye alikiri kuwa zamani kulikuwa na majaribio mengi ya mapinduzi nchini humo, lakini sasa walikuwa na amani ya kutosha kiasi cha kupata usingizi bila hofu.

"Siku za nyuma tuliyapitia (majaribio ya mapinduzi), lakini sasa mioyo yetu imetulia. Lala ukijua kwamba kesho utaamka salama na kwenda kazini kwako kama kawaida" alisema.

Aidha, kwa mujibu wa BBC, Septemba 30, 2023, siku moja kabla ya kuwasili kwa Rais Ndayishimiye kutoka UNGA, Wizara ya Mambo ya ndani ilikanusha uvumi huo na kuwataka watu kuupuuza.

Nchi ya Burundi ina historia ya kukubwa na majaribio ya mapinduzi yapatayo 11 ambapo jaribio la mwisho lilifanyika mwaka 2015 wakati Rais wa nchi hiyo Hayati Pierre Nkurunziza alipokuwa nchini Tanzania kwa ziara maalum.

Evariste Ndayishimiye aliingia madarakani kuongoza nchi ya Burundi mnamo Juni 18, 2020 baada ya kushinda uchaguzi wa Mei 2020 uliofatiwa na kifo cha mtangulizi wake Hayati Pierre Nkurunziza.
Tetesi mbaya za Burundi hutolewa na team ya Rwanda inayochafua Burundi, au kundi la wakimbizi wa kisiasa wa Burundi hasa wanaoishi Rwanda.
Unaweza kuta hamna lolote lililotokea ila ni kama leo hivi Rais kabadilisha mawaziri wizara nne za kawaida. Vijana na elimu, afya, mambo ya nje na nyingine.
 
Tetesi mbaya za Burundi hutolewa na team ya Rwanda inayochafua Burundi, au kundi la wakimbizi wa kisiasa wa Burundi hasa wanaoishi Rwanda.
Unaweza kuta hamna lolote lililotokea ila ni kama leo hivi Rais kabadilisha mawaziri wizara nne za kawaida. Vijana na elimu, afya, mambo ya nje na nyingine.

Hayo maneno inasemekana rais wa burundi ndo ameyasema
 
Burundi inatakiwa iwe na raisi mtusi ndo iwe na maendeleo kama Rwanda wahutu hawana akili za kimaendeleo
 
Back
Top Bottom