Yeah ni kweli wachagga wameshakuwa na dola yao kamili la kujitegemea kabla ya uhuru wa Tanganyika na hata ukoloni history inaeleza wazi jamaa hawajaibukia juzi na wa muda mrefu sana kwenye maendeleo.
Ukibahatika kutembelea Moshi interior utastaajabu sana na utajua tu wachagga waliendelea tokea muda mrefu. Kuna nyumbani kwa mzee fulani Marangu niliingia mgombani huko nikakuta ndani kwake ana frames za ukutani
Zenye pictures na painting za mapapa wa kikatoliki kuanzia wa miaka ya 1800 amezitandaza kuanzia kwenye veranda ya nyumbani kwake mpaka ndani na anasema hizo pictures amemkuta nazo babu yake pamoja na vitu vingine.
Jiulize wakati huo maeneo mengine walikua wapi?