Movic Evara
Senior Member
- Jan 31, 2018
- 197
- 431
Hii ngoma ya DRC bado mbichi. Na moja kati ya mambo yanayozorotesha maridhiano ni pande zinazotuhumiana kugoma kukutana. Wataalamu wa Conflict resolution & mediation wanasema ukiweza kuzikutanisha pande mbili zinazosigana, tayari umeshasolve mgogoro kwa 50%. Sasa shida kubwa ya mgogoro wa DRC ni kwamba wale Key Stakeholders wanakwepana. Kagame akihudhuria kikao cha maridhiano, Tshisekedi anakula chocho. Na Tshisekedi nae akihudhuria Kagame anaweweseka na kuyeyuka kiwendawazimu kama ndugu yangu @joramnkumbi. Sasa mgogoro utaishaje?
Tangu walipokutana Nairobi mwezi December 2022, hadi leo hawajakutana tena uso kwa uso. Wanatuhumiana lakini wanakwepana. Na hii inafanya mgogoro kuwa tete zaidi. Sasa leo ndo ilikua siku ya kuvunja fitna. Wengi walikua wanajiuliza je watakutana? Media kubwa duniani kama BBC, DW na Aljazeera zimesubiri kwa bashasha kuona kama mafahali hawa wawili watakutana leo jijini Dar Es Salaam. Kagame na Tshisekedi wote walidhibitisha kushiriki mkutano wa leo.
Lakini kama ilivyo destiri, Kagame katinga Dar, Tshisekedi katuma mwakilishi. Ikumbukwe Mkutano wa Nairobi ambao ulishindikana kufanyika, Tshisekedi alikua tayari kwenda lakini Kagame akasusa. Je nani atafanikiwa kuwakutanisha mafahali hawa uso kwa uso ili kuokoa damu zisiendelee kumwagika mashariki mwa Congo? Je kikao cha leo kinaweza kuleta matumaini yoyote ya amani bila uwepo wa Tshisekedi? Tukutane saa 1 tuendee na simulizi yetu kuhusu mgogoro wa DRC. Andaa popcorn, zisiungue sana.!