Rais wa FIFA kutua Tanzania wiki ijayo,muda huohuo Kenya watampokea Raila Odinga

Rais wa FIFA kutua Tanzania wiki ijayo,muda huohuo Kenya watampokea Raila Odinga

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
Mwishoni mwa wiki hii Raila Odinga atasifiri nje ya nchi ambapo anategemewa kurudi trh 22 huku maandalizi makubwa ya mapokezi yakirajiwa kufanyika wakati huohuo Dar es Salaam itampokea rais wa FIFA.
Tiririka nayo hapa chini,kwa hisani ya Zanzibar24.co.Tz
Tanzania inataraji kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA (Fifa Summit) utakaofanyika February 22, 2018 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

Mkutano huo mkubwa wa pili unaofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania unashirikisha nchi 19 Wanachama wa Fifa.

Mkutano huo utakaoongozwa na Rais wa FIFA Gian Infantino pia utahudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) Ahmad Ahmad, Makamu wa Rais wa Fifa,Katibu mkuu wa Fifa na viongozi mbalimbali wa FIFA na CAF ikiwemo wajumbe wa kamati ya utendaji.

Wageni kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano huo wataanza kuwasili Tanzania Februari 20, 2018

Ajenda za mkutano huo mkubwa wa Fifa ni miradi mbalimbali ya Fifa zamani ikifahamika kama Goal Project na sasa ikifahamika Fifa Forward Programme,ajenda ya soka la vijana,Wanawake na klabu wakati ajenda nyingine ya mkutano huo ni kujadili kalenda ya kimataifa ya Fifa,kuboresha masuala ya uhamisho na vipaumbele vyake

Nchi zitakazoshiriki ni Bahrain,Palestina,Saudi Arabia,Umoja wa Falme za Kiarabu(UAE),Algeria,Burundi,Africa ya Kati,Ivory Coast,Mali,Morocco,Niger,Tunisia,Bermuda,Monserrat,St,Lucia,Us Virgin,Maldives,Congo na wenyeji Tanzania.

Akizungumzia Mkutano huo unaofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania Rais wa TFF Ndugu Wallace Karia alisema TFF inajivunia kupata uwenyeji huo mkubwa wa mkutano wa FIFA na hiyo inachangiwa na mahusiano mazuri na wadau mbalimbali ambayo yamezaa matunda.



Rais Karia ameongeza kuwa hiyo ni fursa kubwa kwa Serikali kupitia Wizara zake kuweza kutumia fursa hiyo ambayo inaweza kusaidia katika upande wa Uchumi
 
Akili zako unazielewa wewe mwenyewe! FIFA na Raila, wapi na wapi? Sawa tu na watz wakimpokea Tundu Lissu huku wakenya tukiwapokea wanariadha wetu na medali zao. Au timu yetu ya raga, Rugby 7's wakitoka ughaibuni kufanya yao. Havihusiani hata kidogo!
 
Akili zako unazielewa wewe mwenyewe! FIFA na Raila, wapi na wapi? Sawa tu na watz wakimpokea Tundu Lissu huku wakenya tukiwapokea wanariadha wetu na medali zao. Au timu yetu ya raga, Rugby 7's wakitoka ughaibuni kufanya yao. Havihusiani hata kidogo!
we hujaelewa kitu yaan wakenya watakuwa wanampokea raisi wao huku raisi mwingine akiwa amelala pale statehouse!![HASHTAG]#maajabuyakenya[/HASHTAG]
 
Raila Odinga hajakamatwa tu kwa makosa ya uhaini?
 
Back
Top Bottom