Rais wa G-Bissau ashambuliwa nyumbani

Rais wa G-Bissau ashambuliwa nyumbani

Ladslaus Modest

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2008
Posts
635
Reaction score
27
Shambulio la kufyatuliana risasi nyumbani kwa rais wa Guinea-Bissau kumesababisha mtu mmoja kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa, sasa chache baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliopo nchini humo umethibitisha kuwa JRais Joao Bernardo Vieira hakudhuriwa katika shambulio hilo liliotokea usiku.

Shambulio hilo lilihusisha askari kufyatua risasi katika nyumba ya mkuu huyo wa nchi.

Umoja wa Afrika umetoa onyo dhidi ya jaribio lolote la kuchukua madaraka kwa nguvu katika nchi yenye historia ya kufanya mapinduzi katika siku za hivi karibuni.

Iliyokuwa chama tawala nchini humo kimeshinda nafasi za ubunge kwa kiasi kikubwa.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya Afrika ya Magharibi, Will Ross alisema shambulio hilo linaonyesha kuwa ni jaribio lilioshindikana la kupindua serikali hiyo.


chanzo: BBCSwahili.com | Habari | Rais wa G-Bissau ashambuliwa nyumbani
 
Ila huyo jamaa nae ni kama vile anakula deal na mafia wa Drugs hapo west Africa

Tusubiri mapinduzi mengine very soon hapo DRC maanake kabila si kamtimua kazi mkuu wa Jeshi? Na jeshi lenyewe halina nidhamu kabisa.Africa tuna taabu
 
Back
Top Bottom