Rais wa Guinea Bissau awatishia maafisa wa Ecowas waliokwenda kuzungumzia tarehe ya uchaguzi, waamua kuondoka nchini humo

Rais wa Guinea Bissau awatishia maafisa wa Ecowas waliokwenda kuzungumzia tarehe ya uchaguzi, waamua kuondoka nchini humo

Strong ladg

Senior Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
170
Reaction score
445
Mnamo tarehe 1 Machi 2025, maafisa wa ECOWAS waliotumwa nchini Guinea Bissau kuzungumzia tarehe mpya ya uchaguzi walilazimika kuondoka nchini humo baada ya vitisho kutoka kwa Rais Umaro Sissoco Embalo.

Uchaguzi nchini Guinea Bissau ulipaswa kufanyika Novemba 2024 lakini Rais Embalo ametangaza kuwa uchaguzi utafanyika Novemba 2025. Wakati huohuo wapinzani wanadai utawala wa Rais Embalo ulipaswa kufikia kikomo mnamo mwishoni mwa mwezi Februari 2025 ingawa mahakama kuu imemruhusu akae madarakani hadi mwezi Septemba 2025.

Kutishiwa kwa maafisa wa ECOWAS kunazusha maswali kuhusu nguvu na ushawishi wa jumuiya hiyo ndani ya nchi wanachama huku ikiwa ni miezi miwili pekee imepita tangu Niger, Mali na Burkina Faso wakome rasmi kuwa wanachama wa ECOWAS.

Hadi sasa Rais Embalo hajazungumzia tukio hilo na ECOWAS haijatangaza hatua zitakazochukuliwa ili kurejesha demokrasia nchini Guinea Bissau. Jumuiya ya ECOWAS hutumia vikwazo au hata kupeleka wanajeshi ili kurejesha demokrasia ndani ya nchi mwanachama.

20250303_181637.jpg
 
Si ameona kuhusu Kongo kua aina meno iyo jumuiya.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Hao maafisa ilitakiwa watandikwe bakora kabisa kiherehere tu
Unaenda kuhangaika na mambo ya nchi nyingine ili hali matatizo yetu waafrika ni kama yanafanana
 
Back
Top Bottom