Rais wa Horoya asema Simba ni timu ndogo yenye kelele nyingi mitandaoni

Horoya fan

Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
79
Reaction score
253
Raisi wa klabu ya Horoya ya nchini Guinea bwana Soufiane Antonio Souaré ameshtushwa na habari alizokutana nazo hapa nchini kuwa klabu ya Simba ni klabu kubwa barani Afrika.

Raisi huyo amesema kuwa yeye pamoja na watu wote wanafahamu klabu kubwa Afrika ni Al Ahly, Zamalek, Esperance, Wayda, Raja Casablanca, TP Mazembe, Mamelodi Sundowns, Far Rabat, Js Kabylie na pa bwana Antonia akasema hata klabu kama Es Setif, Enyimba, Asec mimosas, Asante kotoko, Stella Abidjan, Kaizer chief, Orlando pairate, Canon Younde, As Vita club, Ismaily, Etoile du Sahel, Club Africaine, na Hearts of Oak zimewaacha mbali Simba Kwa mafanikio.

Simba kwao klabu zote hapo juu zimewahi kubeba ubingwa wa vilabu barani Afrika.

Raisi huyo amemalizia kwa kusema anasikia kelele nyingi mtandaoni za mashabiki wa simba zinazoihusisha Simba na vilabu vikubwa lakini haioni miongoni mwa vilabu vikubwa hapa barani Afrika.

 
Sababu ukubwa ameupima kwa kuchukua kombe asipingwe.

Ila the fact kuwa anazisikia habari za simba na kuzizungumzia ni suala la muda tu maana mashindano bado yapo kila mwaka.
 
Ndugu mwaandishi wa Aston villa na Man City Nani anamzid mwenzake mafanikio hivi karibuni au Nani ni mkubwa??
 
ukubwa wa club unaupimaje?

by the way simba sio kubwa barani africa ila ni tishio kwa baadhi ya vilabu vikubwa africa

pia mwambie ukweli unaouma kuwa Simba ni kubwa kuliko hao Horoya

mimi naongea kama mwananchi damudamu tena mzee wa kijiweni wale wazee wa Hakunaa hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…