Rais wa Ivory Coast awafukuza wanajeshi wa Ufaransa nchini Ivory Coast

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara ameamuru Wanajeshi wa Ufaransa nchini mwake kuanza kuondoka kuanzia Januari hii.

Katika ujumbe wake mnamo Desemba 31, 2024, Rais Ouattara amesema “tumechukua uamuzi kwamba Wanajeshi wa Ufaransa waanze kuondoka Côte d’Ivoire kwa njia iliyopangwa.”

Ufaransa ina takribani Wanajeshi 600 nchini Ivory Coast. Katika nchi nyingine Wanajeshi wa Ufaransa waliosalia ni 1,500 nchini Djibouti na 350 nchini Gabon.

Hali hiyo hasi ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na ukweli kwamba Ufaransa imezishutumu serikali za mpito za nchi hizo kwa kufanya kazi na kundi la kigaidi la Wagner lenye makao yake nchini Urusi, ambalo linashutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu
 
Kwa nini hao Wanajeshi wa Ufaransa walikuwepo kwenye nchi hiyo at the first place? Na kwa nini sasa anataka Wanajeshi hao waondoke kwenye nchi hiyo?
Awe mwangalifu, asifanye maamuzi kwa pupa na kwa kukurupuka, itamgharimu sana. Laurent Gbagbo yupo huru tayari ameachiwa huru na Mahakama ya ICC, asije akapishana naye tena katika milango ya Ikulu yeye Ouattara akiwa anatoka na Laurent Gbagbo akiwa anaingia Ikulu.
 
Hawa wanajeshi wa ufaransa wanafanyaga nin kwenye makoloni yao
Wana hakikisha Mali wanazoiba zipo salama, wanatoa misaada kwa vikundi vya waasi na magaidi pamoja na kuzipangia nchi walizopo Nini cha kufanya.

Niger wamewafukuza, sasa hivi Uranium yao wanauza wanapotaka wao, mwaka huu Wameshika nafasi ya 3 Kidunia na ya kwanza Africa ukuaji wa Uchumi. Ukuaji wao ni zaidi ya 10%
 
Duuh, bora wafukuzwe tu kumbe
 
Huyo Ouattara si ndiye aliingia madarakani kwa mbinde kwa msaada wa Ufaransa dhidi ya incumbent Laurent Gbagbo? Keshanogewa anajiona naye mbabe!
 
Wawa fukuze tu wapo kwa maslahi ya ufaransa wanyonyaji hata congo sijui wanasubiri nin
 
Huyo Ouattara si ndiye aliingia madarakani kwa mbinde kwa msaada wa Ufaransa dhidi ya incumbent Laurent Gbagbo? Keshanogewa anajiona naye mbabe!
Hajioni mbabe ila anauchungu na rasilimali za nchi yake
 
Back
Top Bottom