- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kupitia ukurasa wake wa X amesema "Kiukweli sijapendezwa na hizi jezi mpya za 2024/2025 maana zinafanana na vijora kwa hali hii nawaahidi wananchi hadi kufikia siku ya Mwananchi tutabadili hizi jezi na kitengo cha ubunifu wa jezi kitapewa onyo kali kwa kuidhalilisha brand ya Yanga"
- Tunachokijua
- Injinia Hersi Said ni mhandisi wa Tanzania na pia Rais wa Klabu ya Yanga (Young Africans Sports Club), moja ya vilabu maarufu vya soka nchini Tanzania.
Leo Julai 29, 2024 kumeibuka ujumbe unaosambaa kuwa Kiongozi huyo wa Yanga hajafurahishwa na jezi Yanga zilizozinduliwa Julai 27, 2024 (soma hapa) huku akidaiwa kutoa onyo kwa Wabunifu wa mavazi hayo Soma (hapa).
Ukweli upoje?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa ujumbe huo si wa Hersi kama inavyodaiwa, bali umewekwa kwenye Mtandao wa X na akaunti inayotaka kufanana na ya Hersi ili kupotosha.
Akaunti rasmi ya Mtandao wa X anayotumia Rais huyo wa Yanga una majina ya Eng. Hersi Said (@Caamil8) wakati ukurasa uliotumika kutengeneza taarifa hii unajitambulisha kwa majina ya Hersi Said (@Caamil_88).
Endelea kutembelea Jukwaa la JamiiCheck.com ili ushiriki kwenye mchakato wa kuhakiki taarifa mbalimbali