Rais wa Kundi la waasi wa M23: Atoa wito kwa waandishi na vyombo vya habari kuwa huru kufanya kazi katika mji wa Goma

Rais wa Kundi la waasi wa M23: Atoa wito kwa waandishi na vyombo vya habari kuwa huru kufanya kazi katika mji wa Goma

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Waandishi wa habari wameambiwa wasiwe na hofu kabisa kuendelea kukusanya taarifa zote katika mji wa Goma!

Waandishi wetu wa Bongo wangeweza hili?
=======================

Rais wa Kundi la waasi wa M23 Bertrand Bisimwa ametoa wito kwa waandishi na vyombo vya habari kuwa huru kufanya kazi katika mji wa Goma na maeneo mengine yanayoshikiliwa na kundi hilo.
.
Akizungumza na waandishi wa habari Bisimwa ameeleza kuwa waandishi hawana sababu ya kuwa na hofu hata wakati wa vita mwanachama yeyote wa kundi hilo hatoweza kumshambulia mwandishi wa habari.

Soma Pia:M23 wasema hawaondoki Goma waapa kuendelea kusonga mbele kuelekea mji mkuu Kinshasa

Aidha amesisitiza wakati wa utoaji wa habari ni muhimu waandishi kuzingatia miiko ya uandishi na kutoa habari kwa kuzingatia usawa kwa pande zote.

Pamoja na hayo amewaambia waandishi wa habari ikitokea kuna yeyyote atakayewasumbua kutoka katika kundi la M23 basi watoe taarifa kwa Bisimwa ili amshughulikie.

 
HIVI LUGHA RASMI YA GOMA NI KISWAHILI?
naona mda wote waongea kiswahili
Ndio, ukanda wote wa mashariki ya Congo wanaongea kiswahili, Goma Bukavu Uvira ni kile kiswahili chao chenye rafudhi ya kikongo. Na ndio kigezo kinacho tenganisha wakongo na wanyarwanda. Rwanda ni kinyarwanda tu!.
 
Back
Top Bottom