Monrovia, Liberia: Rais Boakai akaza misuli, Awasimamisha Kazi Maafisa 457—Wakiwemo Mawaziri, Mabalozi—Kwa Kushindwa Kutangaza Mali.
MONROVIA - Rais Joseph Boakai Jumatano aliwasimamisha kazi zaidi ya maafisa 450 wa serikali kwa kukosa kufuata matakwa yake ya lazima ya kutangaza mali
Picha maktaba : Rais Boakai wa nchi ya Liberia
Rais Boakai alisema kuwa viongozi hao wamekiuka kanuni za maadili ya viongozi wa serikali kwa kutokuwa wazi kuhusu wanachomiliki.
Rais, ambaye aliahidi kupambana na ufisadi alipoingia madarakani mwaka jana, alisema kutotekelezwa kunadhoofisha juhudi za kupambana na ufisadi na kuhakikisha uwajibikaji.
Miongoni mwa waliosimamishwa kazi ni pamoja na mawaziri wa elimu na afya, pamoja na wajumbe maalum wa utalii na uwekezaji.
Pia ni pamoja na maafisa wanaofanya kazi katika Jumba la Serikali, makazi rasmi ya rais, na maafisa wa usimamizi wa kaunti.
Sheria inawataka maafisa wote wa umma kutangaza utajiri wao kabla ya kuchukua nyadhifa zao na wanapoacha nyadhifa serikalini.
Tume ya Kupambana na Rushwa ya Libeŕia (LACC) ilichapisha orodha ya maofisa wote wa umma 457 walioathiŕika, ikibainisha kuwa ilikuwa ikifanya hivyo jinsi ilivyoainishwa na sheŕia.
Boakai, ambaye aliahidi kupambana na ufisadi alipoingia afisini mwaka jana, alisema kushindwa kutii kunadhoofisha juhudi za kupambana na ufisadi na kuhakikisha uwajibikaji.
Februari 13, 2025MONROVIA - Rais Joseph Boakai Jumatano aliwasimamisha kazi zaidi ya maafisa 450 wa serikali kwa kukosa kufuata matakwa yake ya lazima ya kutangaza mali