Rais wa Malawi amuagiza kamanda wa jeshi la nchi hiyo kujiandaa kuondoa wanajeshi wake mashariki mwa DRC

Rais wa Malawi amuagiza kamanda wa jeshi la nchi hiyo kujiandaa kuondoa wanajeshi wake mashariki mwa DRC

Twin_Kids

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2016
Posts
3,692
Reaction score
5,647
Wanajeshi wa Malawi, waliokuwa mashariki mwa DRC, kupitia SADEC, leo wamerudishwa nchini kwao.

Ni katika jitihada za kuhakikisha kusitisha mapigano kati ya serikali na M23 yanafikiwa kwa uhuru. Kuondoka kwao, kutaihakikishia M23 kuwa serikali ina nia ya kuleta amani ya kudumu.

=
BLANTYRE (Reuters) - Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, ameagiza vikosi vya ulinzi kuanza maandalizi ya kuwaondoa wanajeshi wake kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatano.

Wanajeshi wa Malawi ni sehemu ya kikosi cha wanajeshi kutoka jumuiya ya kanda ya Kusini mwa Afrika waliotumwa Kongo kusaidia kukabiliana na waasi wenye silaha. Jumuiya hiyo iliongeza muda wa operesheni hiyo mwishoni mwa mwaka jana.

"Rais Chakwera ameagiza kamanda wa MDF (Jeshi la Ulinzi la Malawi) kuanza maandalizi ya kuwaondoa wanajeshi wa Malawi... ili kuheshimu tangazo la usitishaji mapigano lililotolewa na pande zinazozozana huko na kutoa nafasi kwa mazungumzo yao yaliyopangwa kuelekea amani ya kudumu," ilisema taarifa hiyo.

Source: U.S News
 
..kichwa cha habari chahusika.

..Malawi wamesalimu amri kwa M23.

..Hii maana yake ni kwamba zile mission mbili za kijeshi za SADC nchini DRC zimesambaratika.

..Nini utakuwa uamuzi wa Tanzania, na Afrika Kusini?

..Nini itakuwa future ya ahadi ya nchi za SADC kwamba mwanachama aliyevamiwa atasaidiwa kiulinzi na wanachama wenzake?

..Hatima ya DRC ni nini? Je, DRC inakwenda kugawanywa mapande?
 
Malawi iko upande wa mabeberu toka enzi za ubaguzi wa Africa kusini, hapo watakuwa wamepigiwa simu toka London waondoe majeshi
 
Ushawadanganya watu. M23 wana dhamira yake. Wanavitu wanavyopigana navyo. Hawapigani na kila mtu. Kuondoa jeshi si kuwashinda.
 
Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, amemuagiza kamanda wa jeshi la nchi hiyo kujiandaa kuondoa wanajeshi wa Malawi kutoka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kwa mujibu wa taarifa ya televisheni ya serikali.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa uamuzi huo unalenga "kuheshimu tangazo la kusitisha mapigano", ingawa kusitishwa kwa mapigano kulivunjika baada ya waasi wa M23 kushambulia mji wa Nyabibwe, Kivu Kusini.

Rais Chakwera alikuwa chini ya shinikizo la kisiasa la kuondoa wanajeshi wake baada ya wanajeshi watatu wa Malawi kuuawa katika mashambulizi ya M23 mjini Goma.

Wanajeshi wa Malawi walikuwa sehemu ya vikosi vya kulinda amani vya SADC vilivyotumwa kusaidia mamlaka ya DRC kudhibiti makundi yenye silaha.

Baada ya M23 kuteka Goma, kundi hilo sasa linajaribu kuingia Kivu Kusini, wakilenga mji wa Bukavu. Tayari, waasi hao wameanza kuteua viongozi wao, wakiwemo magavana wa Kivu Kaskazini.

Umoja wa Mataifa umeripoti kuwa takriban watu 3,000 waliuawa katika mapigano ya M23 wakati wa kuuteka Goma, huku kukiwa na hofu ya kuenea kwa magonjwa kama Mpox na kipindupindu nje ya jiji hilo.
 
Mwanajeshi kufia vitani kawaida,hao wanyasa hawana akili
 
Wanajeshi wa Malawi, waliokuwa mashariki mwa DRC, kupitia SADEC, leo wamerudishwa nchini kwao.

Ni katika jitihada za kuhakikisha kusitisha mapigano kati ya serikali na M23 yanafikiwa kwa uhuru. Kuondoka kwao, kutaihakikishia M23 kuwa serikali ina nia ya kuleta amani ya kudumu.

=
BLANTYRE (Reuters) - Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, ameagiza vikosi vya ulinzi kuanza maandalizi ya kuwaondoa wanajeshi wake kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatano.

Wanajeshi wa Malawi ni sehemu ya kikosi cha wanajeshi kutoka jumuiya ya kanda ya Kusini mwa Afrika waliotumwa Kongo kusaidia kukabiliana na waasi wenye silaha. Jumuiya hiyo iliongeza muda wa operesheni hiyo mwishoni mwa mwaka jana.

"Rais Chakwera ameagiza kamanda wa MDF (Jeshi la Ulinzi la Malawi) kuanza maandalizi ya kuwaondoa wanajeshi wa Malawi... ili kuheshimu tangazo la usitishaji mapigano lililotolewa na pande zinazozozana huko na kutoa nafasi kwa mazungumzo yao yaliyopangwa kuelekea amani ya kudumu," ilisema taarifa hiyo.

Source: U.S.News
🇹🇿 na South Africa ndio wamebakia na kiherehere Bora South wao wanaiba Madini sisi tunafanya nini Cha maana? Warudi tuu ,Congo wapambanie mambo Yao.

View: https://www.instagram.com/reel/DFvbBtHJuXG/?igsh=MW9zMmtsNnMycngxOA==
 
inawezekana huyu rais atakuwa ameusoma mchezo kwamba pale kongo kutoboa itakuwa ni ngumu. Kama m23 wanarada na wanamitambo ya kutungulia makombora nk na wanajeshi wa m23 wanapewa posho ya kutosha. Na m23 ni kama kivuli adui ni kagame.
 
Attachments

  • Screenshot_20250207_065233_Chrome.jpg
    Screenshot_20250207_065233_Chrome.jpg
    70.5 KB · Views: 4
Siyo uogq, jiulize Malawi wana maslahi gani na huo mgogoro hadi wakapigane vita?
Hali kadhalika Tanzania, jiulize zaidi ya sifa na kutafuta uadui nini maslahi yetu kwenye vita ya Congo?
Kabla ya mimi kujiuliza peke yangu tujiulize wote.
1. Malawi walifikaje Congo?
2. Kama jirani yako hana usalama elewa hata wewe utakuwa huna, utapokea wakimbizi , uchumi kuyumba kumbuka hawa kuna vitu wanapata tokea kwako
3. Ubinadamu. Huwezi kuina mtu anakatwa kichwa au watu wanaumizana na umekaa tu kwa moyo wa furaha. Utakuwa hauko sawa kiakili
 
Ule mgogoro wa maslahi, Africa kusini ana ujirani gani na Congo? Kuna makampuni makubwa ya SA yanapora madini Congo.
 
Hii ahadi kumbe ipo ?

..hiyo ahadi ipo.

..Na ndio iliyookoa serikali ya Kabila Snr isianguke walipovamiwa mwaka 1998.

..kipindi hicho Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Sadc alikuwa Robert Mugabe.

..yeye alichukua hatua za haraka kutuma majeshi ya Zimbabwe, Angola, na Namibia, kupambana na waasi waliokuwa wakisaidiwa na Rwanda, na Uganda.

..sasa hivi Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Sadc ni Rais Samia Suluhu Hassan.
 
M23,wangekuwa hawapendwi kabisa Ile nyomi ya uwanjani Jana wakati wanatangaziwa gavana wao mpya na utawala mpya.... Malawi wamejifunza kitu
 
Back
Top Bottom