Rais wa Malawi ataka Afrika kufutiwa deni

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ameitaka jumuiya ya kimataifa kufikiria kufanya marekebisho na pengine kufuta madeni ya nchi za Afrika.

Akihutubia kikao cha 79 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, rais wa Malawi Lazarus Chakwera alisema nchi za Afrika zinapitia "magumu" katika kutimiza wajibu wao wa kulipa madeni.

"Tunajaribu kila linalowezekana kudhibiti madeni yetu, lakini kama unaweza kufikiria kurekebisha au kufuta kabisa baadhi ya madeni haya, Afrika itakuwa na 'nafasi ya kupumua," Chakwera alipendekeza.

Kulingana na Benki ya Dunia, deni la nje la Afrika liliongezeka kutoka $1.12 trilioni mwaka 2022 hadi $1.152 trilioni kufikia mwisho wa 2023.

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Akinwuni Adesina hivi majuzi alionya katika mkutano wa UN mjini Washington kwamba mikopo "isiyo na uwazi"

inayoungwa mkono na rasilimali inadhoofisha uwezo mkubwa wa kiuchumi wa Afrika, utatatiza utatuzi wa madeni na kuhatarisha ukuaji wa nchi kwa siku zijazo.

Kulingana na Adesina, nchi za Afrika zinatumia asilimia 65 ya Pato lao la Taifa katika kulipia deni la nje.

"Nadhani ni wakati wa sisi kuwa na uwazi wa madeni na uwajibikaji na kuhakikisha kuwa jambo hili lote la mikopo hii isiyo wazi inayofadhiliwa na maliasili inaisha, kwa sababu inatatiza suala la deni na suala la utatuzi," aliongeza.

Hivi karibuni, Benki ya Dunia na serikali ya Marekani wameitaka Malawi "kusimamia ipasavyo" deni lake la nje, ambalo kwa sasa lina jumla ya dola bilioni 4.

Chanzo.Trt Swahili
 
Kama huyu mama kakopa billion 50 Kwa miaka mitatu na hazijulikani ziko wapi?
 
Hamna nchi nyepesi kuongoza kama nchi za kiafrica Tena hususani Tanzania Kwa sababu, hv Raisi wa nchi anatekeleza Kila miradi Kwa kukopa, hv kukopa nayo inahitaji akili kubwa?
Wakishindwa kuendesha Shirika/ taasisi dawa ni kumpa mwekezaji. Hivi kubinafsisha nayo ni kazi ngumu?
 
Katika uongozi wa nchi za kiafrika kuna viongozi wa aina mbili.

1. Puppet leaders
Hawa hutumika na serikali za nchi tajiri kupewa madaraka na kuwanufaisha mabepari na mara nyingi hawa viongozi huwa na hulka ya power mongers, wako tayari kutoa chochote kwaajili ya kupata madaraka.

2. Patriot leaders.
Hawa huwa na moyo wa kizalendo na huwa na mtazamo chanya kwaajili ya maendeleo ya nchi zao, hawa huchukiwa sana na mataifa ya kibepari mana huleta changamoto kwao, hawa mara nyingi hupinga maswala ya kimagharibi hadi kufikia kuwekewa Sanctions kwenye mataifa yao.

Rais Lazarus Chakwera amezungumza kama mzalendo hatamani kuona mataifa ya Afrika yakiangamia kwenda kwenye ukoloni tena kwa sababu ya mikopo kutoka kwenye mataifa kandamizi.

Hatuna namna zaidi ya kumuunga mkono maana wachache wenye mamlaka wakiwa na tabia za viongozi namba moja pale juu wataishia kutuumiza wengi mwishowe tutarudi kwenye zama za utumwa.
 
Mfutiwe madeni wakati hela Mmenunulia Magari ya Kifahali Na Kujenga Mahoteli
 
Ikipendeza riba ziwe kubwa na masharti magumu, maana viongozi wa africa wanapenda kitonga sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…