Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Rais wa Mali Jenerali Assimi Goita amesema jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ( ECOWAS) ni sawasawa na kikundi cha kigaidi.
Rais Goita alitoa kauli hiyo mnamo tarehe 6 Januari 2025 alipokuwa akiwahutubia viongozi wa kimila, kidini pamoja na wale wa asasi za kiraia.
Jenerali Assimi Goita alisema kuwa magaidi wanapokwenda kushambulia mji fulani huzuia watu kutoka na kuingia katika mji huo, vilevile huzuia uingiaji wa vyakula, maji pamoja na dawa.
Kutokana na kwamba nchi za ECOWAS zilifunga mipaka yake pamoja na kuweka vikwazo vilivyokwamisha uingiaji wa bidhaa muhimu kama chakula na dawa katika nchi za Niger pamoja na Mali mara baada ya nchi hizo kukumbwa na mapinduzi ya kijeshi, Rais Goita alisema kwamba ECOWAS walifanya vitendo vinavyofanywa na magaidi huku tofauti pekee ikiwa ni ECOWAS kutotumia silaha kama ambavyo magaidi hutumia.
Rais Goita alihoji iweje vyakula na dawa kwa ajili ya matibabu vizuiwe kuingia kwenye nchi fulani ilihali hata mateka wa vita hupewa chakula, maji na pia hutibiwa pale wanapougua.
Mali, Niger pamoja na Burkina Faso zilitangaza kujitoa kwenye jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ( ECOWAS) mwishoni mwa Januari 2024 mara baada ya kuunda umoja wao waliouita " Alliance of Sahel states"( AES kwa Kifaransa)na kulingana na kanuni za ECOWAS uanachama wao utakoma rasmi mwishoni mwa Januari 2025 ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu nchi hizo zitoe tangazo la kujitoa kwenye jumuiya hiyo.
Vilevile ,mwezi Disemba mwaka 2024, viongozi wa ECOWAS katika mkutano wao uliofanyika Abuja- Nigeria, walitoa taarifa ya kukubali kujitoa kwa nchi za AES kutoka kwenye jumuiya hiyo ingawa walitoa muda wa ziada wa miezi 6 kwa nchi hizo kukubaliwa kuendelea kuwa wanachama wa ECOWAS endapo watabadili mawazo.
Hata hivyo, nchi za Niger, Mali na Burkina Faso zilitoa taarifa ya pamoja ya kupinga muda huo wa ziada wa miezi 6 kwa madai kuwa viongozi wa ECOWAS wanataka kutumia muda huo "kuvuruga amani na usalama" kwenye nchi zao.
Source: YOUTUBE CHANNEL YA SHIRIKA LA HABARI LA MALI( ORTM).
Pichani: Jenerali Assimi Goita