Rais wa Marekani asitisha majadala uliolenga kutafuta suluhu za kunusuru Uchumi wa nchi ambao imeathirika sana kutokana na CoronaVirus

Rais wa Marekani asitisha majadala uliolenga kutafuta suluhu za kunusuru Uchumi wa nchi ambao imeathirika sana kutokana na CoronaVirus

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Rais Donald Trump wa Marekani amesimamisha ghafla majadiliano na chama cha Demokratic juu ya mpango wa kusaidia kupunguza athari za kiuchumi zinazotokana na ugonjwa wa COVID-19, na kuhamishia maamuzi yoyote kuhusu mpango huo baada ya uchaguzi wa Novemba 3.

Trump ameichukuwa hatua hiyo licha ya onyo kutoka kwa mwenyekiti wa hazina ya nchi juu ya hali ya uchumi inayozidi kuwa mbaya.

Rais huyo amesema spika wa Baraza la Wawakilishi, Mdemocrat Nancy Pelosi alikuwa hana nia njema katika majadiliano hayo, na kumuamuru spika wa Baraza la Seneti, Mrepublican Mitch McConnell kuelekeza nguvu zote katika kumuidhinisha mteule wa Trump Amy Coney Barrett kuwa Jaji wa mahakama kuu.

Uamuzi huo unaweza kuwa na athari mbaya kwa kampeni ya Trump kuwania muhula mwingine madarakani, ambyo tayari inapita katika msukosuko mkubwa.

Muungwana blog
 
Back
Top Bottom