Rais wa Marekani Joe Biden, ameiteua rasmi Kenya kuwa mshirika mkuu wa taifa hilo asiye mwananchama wa NATO

Rais wa Marekani Joe Biden, ameiteua rasmi Kenya kuwa mshirika mkuu wa taifa hilo asiye mwananchama wa NATO

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Rais wa Marekani Joe Biden, ameiteua rasmi Kenya kuwa mshirika mkuu wa taifa hilo asiye mwananchama wa NATO.

Hatua hii ina maana kwamba licha ya Kenya kutokuwa katika sehemu ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO, ina ushirikiano wa kina wa kimkakati na usalama na Marekani.

Uteuzi huo unafanyika wiki chache baada ya ziara ya kitaifa ya Rais William Ruto nchini Marekani.

"Kwa mamlaka niliyopewa kama Rais na Katiba na sheria za Marekani, ikiwa ni pamoja na kifungu cha 517 cha Sheria ya Usaidizi wa Kigeni ya 1961, kama ilivyorekebishwa nateua Kenya kama Mshirika Mkuu asiye wa NATO wa Marekani kwa madhumuni ya Sheria ya Kudhibiti Usafirishaji wa Silaha"

Chanzo: itvtz

Marekani akiwa tu Jirani nawe Kiushirikiano tayari kwa 75% una uhakika wa Kufanikiwa kuliko Korea Kusini na Dubai.
 
Back
Top Bottom