‪Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ampa heshima Maxence Melo wa JamiiForums kwenye mkutano wa AU‬

Haiwezekani.

Kuna apps za kutengeneza tweets.

Buhari siyo mwanaharakati mpaka avutiwe na JF.

Sioni Buhari anakutana wapi na JF hadi aijue na amjue mmiliki.
Inaitwaje hiyo app mkuu, nataka nimlishe maneno Trump kuhusu viongozi wa hapa Tz ktk sakata la korosho...
 
Nikumbushe, hivi sisi tuliwakilishwa na nani kwenye mkutano huo? Maana wote nawaona tu bongo
 
Hii ni sehemu ya hotuba aliyotoa Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ...

African Youth must remain the front and centre of restoring traditional African values of probity, integrity, honesty, diligence and hard work.

It is only when the youth drive this change, that corruption will be eliminated.

First, I wish to recognize Mr Moussa Kondo from Mali for his Accountability Lab in the Republic of Mali. He blazed the trail on how to build sustainable coalitions of “Accountapreneurs”.

Secondly, I recognize, Mr Maxence Melo, from the United Republic of Tanzania, founder of JamiiForums for strengthening the viability of whistleblowing policy tools.

I also enjoin us to celebrate our very own Nigerian – Damilola Olawale, founder of Code IT for using technology to give young people the tools to demand transparency in the management of public resources.

You are the unsung heroes of our thematic year of the African Union, the high-impact achievers. You are the REAL AFRICAN CHAMPIONS.

Hongera sana Maxence Melo na timu nzima ya Jamiiforums kwa kazi nzuri mnayoifanya ndani na nje ya mipaka yetu. Mnanikumbusha mwenge uliowashwa juu ya mlima Kilimanjaro Desemba 1961 siku tunapata uhuru kutoka kwa mkoloni. Nikinukuu falsafa ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,,,

"Sisi Watanganyika, tunataka kuuwasha Mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo pale ambapo pana chuki, heshima ambapo pamejaa dharau". Kwa hilo JamiiForums imekuwa mbadala sahihi wa mwenge, inamulika kote.
 
Mkuu umewahi kufika Nigeria? Ni kweli kuna rushwa,lakini Uhuru wa Habari ni mkubwa mno,uchumi ni mzuri mno ,circulation ya pesa ni nzuri hadi raha,nisiongee mengi shortly Nigeria is good ,and Buhari is incomparable to jiwe,yupo social sana
Na saizi Nigeria rushwa imepungua kama kuna anayefuatilia siasa za Nigeria basi waNaija wanalalamika maisha magumu mpk wanasema bora ya ufisadi za tawala za nyuma kuliko hii vita ya ufisadi anayofanya buhari..situation ya Naija ya sasa inafanana na TZ jamaa kila akitumbua na akijinadi kupiga vita rushwa ndipo wafanyabiashara hukimbia

2019 tuone kama ata regain power
 
Mkuu hakuna mfanyabiashara aliyekimbia Nigeria, labda ni hiyo Naija(Niger) unayodai na hali ya maisha si ngumu kama bongo,nilikuwa huko mwaka jana mkuu.

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
 
Ameijuaje jamii forum wakati hajui hata neno Mambo ni nini,inanipa mashaka kidogo yaani magu Leo ausifie mtandao wa misri unaotumia kiarabu ,nadhani jamaa apimwe ni genious sana ,Jamiiforum is big ,maxmelo is a smart leader,ila hii habari big NO
 
Hongereni wna JF woteeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Anastahili pongezi, uwezo wake wa kufikiria melo ni mkubwa sana
 
Wakati Maxence Melo akisifiwa na Buhari kwa kazi nzuri, huku nchini madikteta wanamkalia kooni bila sababu za msingi.. Hata hii kesi ambayo mafisadi wanamsumbua nayo mahakamani alipaswa kupongezwa kwa kuanzisha JF ambamo raia wema hufunguka kuwataja mafisadi wa rasimimali za taifa. Badala yake vibaraka wa mafisadi wamekuwa wakimhangaisha mahakamani kila kukicha. Inauma sana.
 
Hakuna FIRAUNI atakayependa hizi taarifa!!!
MaCCM hawaipendi na hawataipenda kamwe hii taarifa. Huu ni kama msumari wa moto ndani ya kidonda cha mafisadi wa CCM pamoja na vibaraka wao.
 
Katika kurasa wake wa tweeter leo msaidizi wa Rais Buhari katika masuala ya habari Bashir Ahmad ameonesha kauli ya Rais Buhar kumshukuru na kumpongeza sana ndugu Maxence Melo Mkurugenzi wa Jamii forum Tanzania ,kwa mchango wake wa muongozo,elimu na mawazo katika program na Sera waliyoanzisha 2017 Nigeria inayoitwa " Whistle -blowing policy " (Tafsiri isio rasmi).

Sera au Program hii ni ya kupambana na Rushwa,Ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi ambapo Sera hii ina lenga kuhamasisha Raia kwa ridhaa yao kufichua na kutoa taarifa zinazohusu Rushwa,ufisadi,wizi ,ufujaji mali ya umma na matumizi mabaya ya ofisi kupitia wizara ya fedha kwa njia ya mtandao.

Kauli hiyo ameitoa leo Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria katika ikulu yake Mjini Abuja leo wakati wa Launch ya THE AFRICA YOUTH CONGRESS AGAINST CORRUPTION (AYCAC2018),

Maxence Melo aliwahi kualikwa (Umoja wa Afrika)AU kutoa mchango wake namna ya kupambana na Rushwa nchi za barani Afrika, njia bora ya wananchi kushiriki utoaji wa taarifa za ufisadi na rushwa alitoa mfano kama ilivyo Jamii Forum ,na tunaona leo kupitia mchango wa Melo Rais Buhari amempongeza kuwa mchango wake umefanikisha kupanua elimu na ufahamu wa namna ya utekelezaji wa Sera au program yake ya Whistle-Blowing policy nchini Nigeria.

Tanzania ni watu wengi wanatambua mchango mkubwa wa Maxence Melo(Mwanzilishi Jamii forum) katika masuala mengi sana ni watu wachache tuu ndio hujifanya hawajui na kushupaza shingo sababu hiyo ndio maana kesi zisizo na maana zimekuwa zikimuandama.

Jamii forum ni forum kubwa sana ya utoaji taarifa na kuhabarishana ,ina viongozi wengi wa Serikali ingetumiwa na serikali kama Forum ya upataji taarifa za kifisadi na Rushwa na serikali ingetumia hii fursa ya kuhamasisha wananchi kutoa taarifa badala ya kuwaona watoa taarifa kama ni wahalifu , wakosaji au maadui ,

mfano, ushahidi

Tar 19/Nov /2017 niliandika taarifa JAMII FORUM iliyosema "Barua ya wazi kwa Waziri wa madini na kamishna wa madini" nikielezea ufisadi wa afisa madini kanda ya Mbeya,Mikataba mibovu ya wafanyakazi, mateso kwa wafanyakazi.

Taarifa hii Mh.Angela Kairuki aliiona kupitia Jamii Forum na aliniita ofisini kwake nikampelekea taarifa zote ,na mtu aliyekuwa ni fisadi kanda ya mbeya walipokea taarifa yangu na wakaichunguza wakagundua kweli yule mtu ni fisadi akaondolewa ,na maslahi ya wafanyakazi yakaangaliwa vyema .

Maana yangu nini ,ni kuwa tuna njia nyingi za kupambana na ufisadi kwa kushirikisha Jamii, ila sasa hali ilivyo Viongozi wengine ukitoa taarifa utaambiwa umechafua mtu (Defamation), umetoa taarifa ya uongo (Cyber crime act), bila hata kuichukua wakaichunguza.

Hongera sana Kaka Maxence Melo.

Abdul Nondo.
‪Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ampa heshima mwanzilishi wa mtandao wa JamiiForums kwenye mkutano wa AU‬ - JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…