- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
- Tunachokijua
- Kumekuwa na nukuu inayosambaa kwenye mitandao ikidaiwa Rais wa Senegal, Bassirou Faye amekataza watu kuweka picha yake maofisini mwao na badala yake waweke picha za familia zao. (Hapa na hapa)
“Sitaki mbandike picha zangu kwenye ofisi zenu kwa kuwa mimi siyo Mungu na wala siyo kielelezo cha utumishi isipokuwa ni mtumishi tu kwa Taifa badala yake bandikeni picha za watoto wenu ili muwe mnazitazama wakati wa kufanya maamuzi”
Ufuatiliaji wa JamiiCheck.com umebaini nukuu hiyo inayosambaa ni potoshi na haikuwahi kusemwa na Rais huyo kama inavyodaiwa.
Aidha, JamiiCheck imebaini kuwa nukuu hiyo anayohusishwa nayo Faye iliwahi kutolewa na Volodymyr Zelenskyy Rais wa Ukraine mwaka 2019, na iliwahi kuandikwa na mmojawapo wa watumiaji wa JamiiForums.
Endelea kutembelea Jukwaa la JamiiCheck ili uwe karibu na taarifa zilizohakikiwa.