Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amefungua njia kwa wabunge wapya na kuunda bunge lililovunjwa siku ya Jumamosi.
Majina ya wabunge walioteuliwa yalitangazwa kwenye chombo cha habari cha taifa hilo, Shirika la Utangazaji la Sudani Kusini, Jumatatu usiku.
Bunge la sasa linahusisha wabunge kutoka kundi la waasi wa zamani, Sudan People’s Liberation Movement linaloongozwa na Makamu wa Rais wa kwanza Riek Machar na kutoka vyama vingine vya kisiasa.
Kwa mujibu wa makubaliano ya amani ya mwezi Septemba mwaka 2018, vyama mbalimbali vilitakiwa kuchagua wawakilishi wao ili waweze kuteuliwa na rais.
Bunge la Kitaifa la Mpito (TNLA), ambalo lilipanuliwa Jumatatu kutoka wabunge 400 hadi 550, lina wabunge 332 kutoka chama cha SPLM cha Rais Kiir na viti 128 kutoka SPLM-IO cha Bw Machar.
Huku vya ma vingine kama cha South Sudan’s Opposition Alliance (SSOA) viti 50, vyama vingine viti 30 na wafungwa wa zamani viti 10.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, 35% ya viti vinapaswa kwenda kwa wanawake.