Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
TAARIFA KWA UMMA
Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania, Mhe. Zaynab Iddy Kitima ametengua uteuzi wa Ndg. Ibrahim Shukran Aloyce, Naibu Kamishna wa Kamisheni ya Mikopo na Ufadhili.
UFAFANUZI WA RAIS WA TAHLISO
Alipoulizwa na JamiiForums.com kuhusu maamuzi hayo kama yana uhusiano na malalamiko ya Wadau yaliyotolewa juu ya mchakato wa utoaji mikopo hasa kwa Wanafunzi waliokata rufaaa za mikopo, Zaynab Iddy Kitima amesema:
“Hizo taarifa za malalamiko mimi ndio nazisikia leo, kuna masuala ya kinidhamu kwa mamlaka niliyonayo ninapoona kuna jambo linaashiria uvunjivu wa amani au uhamamsishaji wa mambo ambayo ni nje ya Katiba ya ketu sipaswi kuyafumbia macho.”
Pia Soma:
~ HESLB yafafanua madai ya Wanafunzi UDSM kutakiwa kuwa na Kadi ya CCM ili wapate mkopo
~ Wanafunzi UDSM tuliokosa mikopo 2023 na waliopata mikopo kidogo tunaambiwa lazima tuwe na Kadi ya CCM ndio tutahudumiwa