Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
Rais wa Chama Cha Wanasheria wa Tanganyika (Tanganyika Law Society (TLS) Wakili Harold Sungusia amebainisha mambo matatu ambayo wameyagundua ya wananchi wa Tanzania na baadhi ya viongozi kuhusu katiba iliyopo sasa kwa mikoa ambayo wamefanya mikutano.
Amesema kuwa Miongoni mwa mambo ya msingi ambayo wameyagundua ni kwamba yapo makundi matatu ya wananchi wa Tanzania na baadhi ya viongozi.
Ameyataja makundi hayo matatu ambayo ni wale wanaosema katiba ya sasahivi haina tatizo lolote tusipoteze muda tuendelee na maisha yetu.
Kundi la pili ni wale wanaosema katiba iliyopo ina dosari kadhaa ambazo tunaweza kuzirekebisha tukaenda mbele na kundi la tatu ni wale wanaosema katiba iliyopo haifai kabisa inahitajika katiba mpya ambayo itasaidia nchi kwenda mbele.
Wakili Sungusia amesema hayo leo Juni 22,2024 jijini Dodoma wakati akizungumza na vyombo vya habari kwenye mjadala wa wazi juu ya mchakato wa kupata katiba Mpya Tanzania.
"Wananchi wana maoni mengi lakini ukisikiliza kwa haraka utagundua kwamba wamesikitishwa na kilichotokea mwaka 2014 baada ya ile tume ya katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Warioba kumaliza kazi yake"amesema
Aidha amesema kuwa miongoni mwa mambo ambayo wamejiuliza ni kwamba kwa nini mchakato uliopita ulikwama.
"Usipojua ulipoangukia na kilichokusababisha ukaanguka,huwezi kuchukua tahadhari kwa hatua unazoenda mbele,tulikwama kwenye mchakato uliopita kwa sababu ya mgongano wa maslahi,waliokuwa nje ya Utawala walidhani kwamba watatumia katiba kuweza kuingia madarakani na waliokuwa madarakani walidhani watatumia mchakato wa katiba kuendelea kubaki madarakani"amesema
"Sisi tunataka katiba ya Wananchi siyo katiba ya makundi fulani katika nchi hapana,ni katiba ya raia wote wajisikie katiba ni ya kwao kwa utaratibu huo tunapendekeza mchakato utakaofata wakupata katiba ya Wananchi usimamie umahiri wake suala la mgongano wa maslahi.
Pia amesema kuwa watakaohisika katika kutaandalia mchakato wa katiba wasihusike Katia kugombea nafasi zozote za Kisiasa.
Katika hatua nyingine Wakili Sungusia amezungumzia suala la mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino yanayoendelea nchini amesema kuwa TLS inakemea kwa nguvu zote mauaji ya Albino.
"Ni aibu kubwa kwa Taifa unapotoka nje ya nchi baada ya kuulizwa wewe unatoka kwenye ile nchi yenye visiwa vizuri vya karafu,unaulizwa unatoka kwenye ile nchi inayoua watu wenye ulemavu wa ngozi Albion ni aibu"amesema.
Amesisitiza kuwa kama Watanzania tusikubali hili jambo liendelee na kutoa wito kwa taasisi zote zichukue hatua zinazohitajika kukemea hayo mauaji.
Kwa upande wake Inock Isaya ambaye ni mwananchi mwenye ulemavu wa kuona akizungumza katika mjadala huo wa wazi juu ya mchakato wa kupata katiba mpya amesema kuwa katiba itakayopendekezwa iwazingatie.
"Tungalipenda kuzingatiwa kuwemo kwenye vyombo vya maamuzi bila kujali vyama vyetu,kinyume na katiba ya sasahivi ambayo haitoi hiyo haki,isipokuwa ni utashi tu wa vyama vya siasa na hivyo vyama vya siasa vinawapa watu wachache tena Wanawake na hao Wanawake walemavu hawajachaguliwa na Walemavu wamechaguliwa na watu wa kawaida"amesema
Naye Askofu Mary Madelemo Mwenyekiti wa Wanawake wa Dini mbalimbali Mkoani Dodoma akizungumza kwenye mjadala huo amesema kuwa ni vizuri kuwa na katiba Mpya kwa wakati huu kwa sababu ni wakati wake.
"Tunapoingia kwenye mchakato wa kupata katiba ni vizuri kukayashirikisha makundi yote ili tuwe na lengo moja na mtazamo mmoja"amesema
(Imeandikwa na Manase Madelemu)