Rais wa Tanzania 2030, kipaumbele chako kiwe mipango miji

Atafika?
 
Mipangomiji???!!????
Mbona tumeshachelewa sana.Kwa hatua ya ujenzi holela tulipofikia tumefika stage ya "Point of No Return", Mipangomiji ktk nchi hii haiwezekani tena milele.
 
Njia gani ?
Mipangomiji ni Pure& Applied Science, siyo Siasa, tambua suala hili.
Kwani kuna shida gani hata ikiwa pure applied science? Mbona kuna maeneo imewezekana? Kwa nini isiwezekane sehemu zote?

Ni uvivu tu wa kufikiri na kukosa maamuzi!
 
Mleta mada akili huna asilimia 80 ya watanzania wanaishi vijijini na asilimia 80 ya wapiga kura uchaguzi mkuu wanaishi vijijini hao wa mjini ni asilimia 20 tu kiushindi wa uchaguzi mkuu hiyo agenda Yako dhaifu mno kura ni ku jali walio wengi
 
Mipangomiji???!!????
Mbona tumeshachelewa sana.Kwa hatua ya ujenzi holela tulipofikia tumefika stage ya "Point of No Return", Mipangomiji ktk nchi hii haiwezekani tena milele.
Inawezekana.
Kwanza tunaanza na kuelimisha wananchi kuanzia mtaani, kwamba lazima kila ujenzi Uwe na barabara yenye upana usiopungua mita 10 na eneo la miundombinu mingine hata kama eneo halijapimwa na serikali.
Upimaji Uwe ni huduma kwa wakazi na wamiliki badala ya fikra za mapato kwa serikali.
Pili kuhakikisha uendelezaji wowote wa ardhi kuanzia sasa unakuwa na mpangilio mzuri kupitia elimu hiyo.
Changamoto ni mamlaka husika kutokuwa na uwezo wa kufanya wajibu wake kulingana na mahitaji ya wakati husika.
Tatu, kuwe na mipango endelevu ya uboreshaji wa maeneo yaliyojengwa holela kwa kubomoa na kurekebisha kwa kufidia pale ambapo kuna mahitaji kulingana na soko kwa wakati huo.
 
Narudia tena kusema kwamba haitawezekana kamwe. Je, wewe binafsi umeshawahi kufika kwenye nchi nyingine yoyote ile iliyoendelea yenye Mipangomiji iliyo bora kabisa??Umeshawahi?
 
Hivi ushawahi kujenga nyumba lkn? Unajua maumivu ya kubomolewa?
 
Rais yupi huyo kama waliopita hawajajali hilo kinyume na kupiga jaramba ya siasa na kuteuana! Labda aliyeenda angeweza kwa kiasi fulani na akiwepo shipbuilding Lukuvi mnyalu.
 
Mipango miji sio ujinga ila hakiwezi kuwa kipaumbele nieleweke.
Yaaani miji imekaa kama majalala ya takataka unasema isiwe kipa umbele??? Leo hii kila sehemu mafuriko eti watu wanapoteza maisha kisa mafuriko kwenye makazi ya watu 2023,,,,,kungekuwa na mipango miji ujue hakuna mtu angejenga sehemu ambazo zinauwezekano wakupata mafuriko,,, tembeeni kidogo mkaone miji yawenzenu sio kujifungia kutwa mbagala ranging tatu mnaona dunia imeisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…