Rais wa Tanzania lazima aongoze nchi akiwa Tanganyika?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Tanzania ni Moja chini ya muungano. Kwanini Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania lazima akae bara hata kama ni mzanzibar? Hawezi kukaa Zanzibar na kuiongoza nchi?
 
Wakati wenzio wanasoma na kusikiliza somo la uraia (civics) darasani we kazi yako ilikuwa kusugua punje za ubuyu chini na kuunguza wenzio.

Haya pitia hapa katiba ya nchi upunguze ujinga, wahead kabisa.
 
Attachments

Where is administrative capital for Tanzania??????
Endapo kama Ikulu ya Tanzania itakuwa Zanzibar basi Rais wa nchi naye atalazimika kukaa Zanzibar.
 
No time to read the whole thing; sema ni sura gani na ibara gani na mstari upi hadi upi. Na kwanini iwe hivyo wakati Zanzibar ni nchi sawa na tanganyika?
 
Makao makuu ya serikali yapo wapi mkuu?😁
kuna muungano na makao makuu kipi kilianza? nani kasema makao makuu yawe kule badala ya kule? Kwanini Rais Mzanzibar ahamie ugenini (uncomforted zone) ?
 
Where is administrative capital for Tanzania??????
Endapo kama Ikulu ya Tanzania itakuwa Zanzibar basi Rais wa nchi naye atalazimika kukaa Zanzibar.
Kaka ile haikuwa Ikulu ya Tanzania, ilikuwa Ikulu ya Tanganyika kwaajili ya Tanganyika na mambo yake kama vile ilivyo Ikulu ya zanzibar ilivyokuwa kwaajili ya Zanzibar na mambo yake.
 
Where is administrative capital for Tanzania??????
Endapo kama Ikulu ya Tanzania itakuwa Zanzibar basi Rais wa nchi naye atalazimika kukaa Zanzibar.
Z'zibar hakuna Ikulu kaka? Mbona ile ya Dar ilitumika kwa miaka yooote hiyo bila shida?
 
Je, unaelewa maana ya 'administrative capital for Tanzania?? Ikulu iliyopo Zanzibar ni kwa ajili ya Zanzibar, na wala siyo kwa ajili ya Makao Makuu ya Nchi ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom