Rais wa TFF asipodhibitiwa kuna siku atapeleka mechi ya Simba Vs Yanga uwanja wa Kinesi au Bandari

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Mimi kwetu ni Tanga, nimezaliwa Ocean Road pale Ilala lakini babaangu ni mdigo wa Mwakidila ila ameniachia nyumba pale Mabawa, nina ndugu Chumbageni, Commercial, Mikanjuni, usagara na Duga.

Tanga hakuna uwanja mzuri wa kuushinda uwanja wa Chamazi, kusema ngao ya jamii unaipeleka Tanga kwa kigezo kipi?

Tanga kuna nini maana washabiki wenyewe Tanga hawana msisimko tena na mpira tangu African Sports na Coastal zikose mvuto.

Mechi ya Simba na Yanga ikachezwe Tanga wakati mechi ya fainali Yanga vs Azam tumeshuhudia mashabiki wachache uwanjani, uwanja umekosa kabisa msisimko.

Kwanini Karia aaachwe awe anajifanyia tu anavyotaka, umefanya tathmini gani hasa upeleke gemu hiyo Tanga, hata kama unadai Tanga japo siamini kwa sura yako navyoiona lkn Tanga hakuna mvuto kupeleka mechi za hisani.

Vilabu hivi vikae na TFF vikubaliane na sio TFF kuburuza buruza tu.
 
Tanga kuna msisimko mkubwa tu wa mpira haswa kwa timu wanazozipenda mfano Coastal union, African Sports na Simba Sc mfano uliotolea wa mechi kati ya Azam na Yanga ni kweli hakukuwa na hamasa kubwa hivyo kutokana na klabu ya Yanga kutokuwq na mashabiki wengi jijini humo
 
Ni kweli YANGA haiwezi kupendwa na **WACHAWI.
 
Hivi muda wa Karia kuisha uongozi wake ni lini?

Maana huyu mtu hatakiwi pitisha hata sekunde moja ofisini.
Huyu jamaa amalize muda wake, atembee ili mpira urudi mikononi mwa wenye mpira wao. Enzi za Leodgar Chilla Tenga, TFF iliheshimika sana.

Walipokuja hawa wanasia (Jamal Malinzi, na huyu Karia), ndipo nongwa ilipoanza. Majungu, siasa, kukomoana, kuchafuana, na upigaji ndiyo vimetawala.
 
Huo ndio ukweli..pia akumbuke mechi hiyo ya Ngao mashabiki wa Dar na mikoa ya jirani watakuwepo kwa wingi pia.
 
Mmeanza kutafuta visingizio
 
Upo sahih Mtoto wa kitanga


Kwenye hili Mimi nipo nyuma yako Wallah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…