Rais wa TFF, Jamal Malinzi, kuzungumza na Vyombo vya habari Kesho Juni 23, 2015

"Nimshukuru kocha kwa jitihada zake zote licha ya matokeo kuwa mabaya. Hata hivyo haimaanishi kocha hakujitoa kwa moyo wake wote...
 
Swali: Kwa nini ulimfukuza Kim Poulsen kwa haraka haraka?
Jamal Malinzi: Tuambiane ukweli. kilichompata kocha Nooij ndicho kilichomkuta Kim Poulsen. Nyie ndie mlikuwa mstari wa mbele kuandika Kim Poulsen amefikia mwisho wa uwezo wake, na magazeti yapo"
 

kwa hio yeye anafuata ushauri wa magazeti....? bomu kabisa huyu
 
Kwahiyo anajiuzuru au bado anakomaa kama Nkurunzinza?
 
" Watanzania tusidanganyane; Bila uwekezaji kwenye soka la vijana hatuwezi kufika popote " Jamal Malinzi, Rais wa TFF.Kikao ndio kimeanza

Swali : Je, unamtazamo gani kuhusu msingi aliouacha Tenga. Unadhani tulikuwa na uelekeo sahihi ama la.
 
Tumechoka na wimbo wa "kuwekeza kwenye soka la vijana. " Sasa tunahitaji mtendaji
 
Mimi nasema : Watanzania tusidanganyane, bila kuchagua viongozi wenye weledi mkubwa na nia ya dhati kukuza soka letu,hatufiki popote.
 
ooh, ni marufuku serikali kuingilia maswala ya mpira! FIFA wawakatalie wanaume wa CIA na FBI basi kama ni wanaume kweli, kamata chain yote ya FIFA, CAF, Malinzi nk weka jela! nyambaf!
 
Wakati tukiendelea kumnanga huyo Mlinzi, tuchukulie hii kama 'chorus' huku tukitafakari!
 
Huyu malinzi alikuwepo jf kwa jina la bishanga baada yajf kumsaidia kuipata tff akasepa na hata ule uzi wake wa maswali na majibu akaukimbia. Asepe tu hana mpango kazi wowote zaidi yakuiba hela
 
Wakati tukiendelea kumnanga huyo Mlinzi, tuchukulie hii kama 'chorus' huku tukitafakari!

Dah, ujumbe murua kabisa uliobeba ukweli mchungu. Lakini yote katika yote tunahitaji mahali pa kuanzia. Tupate viongozi wenye maono na si maneno mengi na ujanja ujanja. Vinginevyo nitaendelea kushikilia msimamo wangu bora kabisa ; tutafute kiongozi wa soka toka nchi za ulaya (mfano mstaafu wa FA) aje tumkabidhi TFF. Alete na watendaji muhimu anaowahitaji halafu tumpe jukumu la kutuinulia soka letu. Huyu atakuwa hajui Simba wala Yanga wala Azam, anachojua ni taratibu na sheria za soka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…