Rais wa TFF, Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu Celestine Mwesigwa washikiliwa na TAKUKURU

Hii zama nyingine bana, hakuna kupepesa macho. Tanzania yenye Neema iko njiani, Tanzania bila ufisadi inawezekana. Hongera Baba Magufuli
 
Ni sahihi kabisa mkuu, amekuwa na tatizo la upendeleo ktk ajira. Ndio maana nasisitiza kuwa baadhi ya matatizo yake yanarekebishika.
Soon atatengeneza Kagera Star[emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Ili iweje? ktk ubinadamu hakuna aliyekamilika kama ulivyo wewe au mimi. Jamal ana mapungufu yake pia kama mwanadamu mwingine.
Nchi hii sometime unaweza kushindwa kuelewa wakati wa kuwa serious au wakati wa kutimiza 'melengo' fulani fulani. Sio ajabu ukasikia kuwa alijenga uwanja wa golf kijijini kwake kwa pesa za tff!
 
Nchi hii sometime unaweza kushindwa kuelewa wakati wa kuwa serious au wakati wa kutimiza 'melengo' fulani fulani. Sio ajabu ukasikia kuwa alijenga uwanja wa golf kijijini kwake kwa pesa za tff!
Tunaweza tukawa na nia moja, lakini tukapishana mitazamo ktk kufika pale tunapopataka.
 
Nchi hii sometime unaweza kushindwa kuelewa wakati wa kuwa serious au wakati wa kutimiza 'melengo' fulani fulani. Sio ajabu ukasikia kuwa alijenga uwanja wa golf kijijini kwake kwa pesa za tff!
Ndio maana tumeletewa JPM...tuache huu wizi wizi bila aibu
 
Dead & buried[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Hii kama ni kweli basi Jamali malinzi naye atakuwa ni kilaza kupita kiasi aisee, hivi yeye bado tu hajashtuka kwamba hizi ni zama zingine kabisa. Hapo ukute wazee wa usalama washafanya yao.
Mmhh Blazaaa usalama tena..
 
Ungetusaidia kuorodhesha hayo mengi aliyoharibu walau tuyajue.
Kama ni mdau wa soka la Tanzania unapaswa kuyafahamu madudu aliyoyafanya Malinzi tangu aingie TFF nahisi hata nikikutajia utaanza kuyapinga moja moja,nakupa haya machache

1.Kuhamisha ofisi za TFF toka Karume hadi Posta
2.Kuajiri/kuteua viongozi wajumbe wa kabila lake tu
3.Kuwafungia kwa muda mrefu wadau wa soka waliokuwa wanampinga waziwazi (Dr Ndumbaro)
4.Kiwango cha Taifa Stars kuzidi kuporomoka
5.Ubadhirifu mkubwa wa fedha
6.Upangaji wa matokeo
7.Program mbovu za timu za taifa(Maboresho)
8.Kuvunja mikataba ya Kim Poulsen na kumlipa fedha gharama za kuvunja mkataba(baadae aligundua amekosea akamrudisha na ndio ammesaidia mafanikio ya Serengeti Boys)
 
Tunaweza tukawa na nia moja, lakini tukapishana mitazamo ktk kufika pale tunapopataka.
Sijui ni wangapi tunaelewa kwa ufasaha ulichokiandika, binafsi naona kila mmoja wetu angelijua hili! Umeandika kitu cha msingi sana.
 
Hzo zote ni dhana ndg. We umeona kuna ubaya gani kuhamisha ofisi za shirikisho? Matokeo yapi yaliyopangwa? Kushuka kwa viwango vya stars ni suala la ufundi, ndio maana wameona njia bora ya kunusuru soka letu ni kuwekeza kwa vijana kama walivyofanya wenzetu mataifa yaliyoendelea. Ubaguzi wa kikabila hata me sikubaliani naye, japo ipo hvyo taasisi nyingi tu duniani. Kuhusu ubadhirifu, siwezi kusema chochote maana me sijaona ushahidi wowote wa kudhihirisha hayo. Jambo lingine muhimu ni kujua kuwa maamuzi ya raisi wa shirikisho ktk mambo ya ufundi sio wa mwisho. Kuna kamati ya utendaji na sekretarieti yake ambazo zinafanya kazi nyingi sana kwa pamoja.
 
Sijui ni wangapi tunaweza kuelewa kwa ufasaha ulichokiandika, binafsi naona kila mmoja wetu angelijua hili!
Tatizo ni uandishi au Tatizo ni nini mkuu? Sijakuelewa aisee, unaweza kunisahihisha pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…