Sasa TAKUKURU inafurahisha wananchi. Inaonesha sasa hakuna aliye juu ya sheria
Kama TAKUKURU watamgusa kila aliyefanya ufisadi na wizi wa mali ya umma, watapongezwa. TAKUKURU wanapaswa kujua kuna mfanyakazi mmoja wa umma ni kama ameshindikana. Anatumia kila aina ya ushawishi ikiwa ni pamoja na kuhonga baadhi ya watumishi wachache wa TAKUKURU wasio na maadali.
Pia anajulikana kwa kutumia matisho ya waganga wa kienyeji na uchawi ili kutisha baadhi ya watendaji wa serikali wenye imani haba na wanao-ogopa mambo ya kishirikina ili waogope kufuatilia madhambi yaliyofanywa.
Mfanyakazi huyu wa umma aliyeshindikana ni Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha anayejulikana kwa jina la kusomea kama Richardi Joseph Masika ambaye jina lake halisi ni Richard Joseph Mushi.
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zimeonesha kuwa, kwa wakati tofauti katika kipindi cha kuanzia 2010 hadi 2015 zaidi ya TZS bilioni 3 fedha ya Serikali hazijulikani ziko wapi au zilifanyia kitu gani.
Kwa upande mwingine Ndugu Masika au Mushi amewekeza kiasi kingi cha fedha hizo alizoiba serikalini kwenye mali zisizohamishika kama majumba, mashamba na viwanja katika miji ya DSM na Arusha.
hapa chini ni moja ya nyumba aliyojenga Njiro Arusha kwa kutumia fedha aliyoiba serikalini. Pia kwa kutumia madaraka yake alizipatia kampuni zilizofanya kazi ya ujenzi wa majumba yake kazi katika taasisi anayofanyia kazi hali inayoonesha kila dalili za RUSHWA