Rais wa TFF Wallace Karia na Kamati ya Maadili TFF tafadhali msiupokee Msamaha wa Haji Manara kwani ni Mnafiki

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Yaani nikiona Rais wa TFF Wallace Karia na Kamati ya Maadili TFF mmemsamehe Mhamasishaji wa Yanga SC Haji Manara baada ya Yeye leo Kuwaombeni Radhi nitawadharau na Kuwachukia Milele.

Rais wa TFF Wallace Karia nadhani unatambua jinsi Haji Manara alivyokuwa akikukashifu na kuihusisha TFF na Usimba hadi Kuwadhalilisha Watendaji wako hapo Karume Ilala.

Rais wa TFF Wallace Karia kuna Mmoja wa Watendaji wako hapo TFF ( Mnazi wa Yanga SC ) baada ya Kujua kuwa Haji Manara anaenda kupata Adhabu Kubwa alimfuata Haji Manara na Kumlazimisha aje Kukuona ili Kukuomba Radhi Kinafiki ili uwaombe Wajumbe wa Kamati ya Maadili wasimfungie.

Tafadhali Kamati ya Maadili TFF kamwe msiuamini huo Msamaha wa Haji Manara kwani ni wa Kinafiki tupu na anewawahi Kuwaomba Radhi ili hata Mkimfungia apate Huruma ya Wafuasi wake wengi Wapumbavu kuwa mmemuonea kwani aliwaombeni Msamaha.

Haji Manara ni Jeuri, Kiburi, Mshamba na ana Dharau zisizovumilika hivyo tupieni mbali huo Msamaha wake na mpeni Hukumu ya kuwa Fundisho wa Wapuuzi wengine wa Mfano wake.
 
Kama kamati ya maadili ikimsamehe Manara basi itawalazimu wawasamehe na wengine wote iliowafungia, akiwemo Shaffih Dauda, muhimu nao waombe radhi.
Shaffih ali omba msamaha lini?
 
Kama kamati ya maadili ikimsamehe Manara basi itawalazimu wawasamehe na wengine wote iliowafungia, akiwemo Shaffih Dauda, muhimu nao waombe radhi.

Manara ameomba radhi kwa kosa la kujibizana na Rais wa TFF.

Huyo shaffih Dauda alipewa muda wa kuomba msamaha ila alikaidi. Ataendelea kubaki kifungonu.



[Picha Haihusiani na Comment]
 
Jambo limeisha hilo...... Huyo Manara atapigwa faini na Yanga itapigwa faini kwa kosa la mashabiki wake kufanya vurugu

Manara ataendelea kuwakera watu kwa miaka mingi zaidi
 
Manara ameomba radhi kwa kosa la kujibizana na Rais wa TFF.

Huyo shaffih Dauda alipewa muda wa kuomba msamaha ila alikaidi. Ataendelea kubaki kifungonu.

View attachment 2281883

[Picha Haihusiani na Comment]
Wakimfungia Manara adhabu imuhusu pia msomali maana Manara hakujibizana na upepo
 
Raisi naye anatakiwa kuwa na kesi ya kukosa maadili nae afikishwe kwenye kamati hatuwezi kuwa na raisi ambaye anazozana na wasemaji wa timu...Raisi huyo hana adabu
 
Huenda walisoma hili andiko kabla ya kutoa adhabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…