Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
PARIS, UFARANSA
RAIS Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema kuwa kauli yake kwamba Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) limepatwa na kifo cha ubongo ilipiga kengele ya hatari kwa nchi wanachama na kwamba hataomba radhi kwa kutoa matamshi hayo.
Matamshi hayo makali ya Rais Ufaransa yamepokewa kwa hisia kali na viongozi wenzake wa nchi za Ulaya wanaosisitiza kwamba, nchi za bara hilo zingali na haja ya kutegemea muungano huo wa kijeshi katika masuala ya ulinzi.
Hata hivyo Emmanuel Macron ambaye alikuwa akizungumza kandokando ya Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema hataomba samahani kwa matamshi yake ambayo amesema yalihitajika baada ya wanachama wa NATO kuelekeza mazingatio yao zaidi katika masuala ya bajeti ya shirika hilo badala ya masuala ya jiografia ya kisiasa.
Amesema aliuliza maswali ambayo hayakupatiwa majibu ambayo ni pamoja na kuhusu amani barani Ulaya, hali ya baada ya kuvunjika Makubaliano ya Silaha za Nyuklia za Masafa ya kati (INF), uhusiano na Russia na kadhia ya Uturuki na kuhoji ni nani adui?
Rais wa Ufaransa amesisitizia kuwa hataomba samahani kwa kusema kuwa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi NATO limepatwa na kifo cha ubongo.
Itakumbukwa kuwa mapema mwezi huu Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alieleza wasiwasi wake kuhusiana na iwapo Marekani itaendeleza kutekeleza majukumu yake katika Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi NATO na kusema kuwa, shirika hilo limekumbwa na kifo cha ubongo.
Macron alisema kwamba nchi wanachama wa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi NATO pamoja na nchi za Umoja wa Ulaya haziwezi kuendelea kuitegemea Marekani kwa ajili ya kujilinda.
Vilevile aliikosoa serikali ya Washington kwa kutokuwa na mawasiliano na wanachama wengine wa shirika hilo katika kuchukuliwa maamuzi ya kistratijia.
Chanzo: ParsToday