Rais wa Uganda, Museveni akutana na Naibu Waziri Mkuu, Doto Biteko

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni amekutana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko Ikulu ya Entebbe nchini humo ili kupokea salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru wa Nchi ya Uganda.

d2d5f3cf-8d95-4987-8689-765dc1e02f29.jpeg
Mhe. Rais Museveni ameishukuru Serikali ya Tanzania na kuongeza kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa na mafanikio makubwa ya kihistoria na kiuchumi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu alikabidhi zawadi kwa Mhe. Rais Museveni kama njia ya kuthamini mchango na ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda.

32ec6e1e-c786-4208-a486-fc7880743dc3.jpeg

6764dca3-20fb-49ae-9207-9c532587642e.jpeg
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stephen Byabato, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe Balozi Stephen Mbundi pamoja na viongozi wengine kutoka ubalozi wa Tanzania nchini Uganda.
 
Dotto anatamba anga za maziwa makuu. Hapo kagame Anazo furaha zote Kwa kuwa ndugu yake dotto mashaka Biteko ni naibu waziri mkuu, na Kulwa masunga Biteko akitarajia kuwa mbunge wa busanda 2025. Masunga Kwa kisukuma ni maziwa fresh
Kagame tena kivipi ? [emoji44][emoji44]
 
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Musekutana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko Ikulu ya Entebbe nchini humo ili kupokea salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru wa Nchi ya Uganda...
Mkutano wa Watusi
 
Nazidi kuuchukia huu muungano.
Nakuelewa.
Lakini nakusihi usiuchukie muungano, wachukie wanaoutumia muungano vibaya. Hawa ndio wanaostahili kuchukiwa na kila mtu mwenye mapenzi na muungano wetu.
 
Naona mseveni kwasasa na viatu ni vitu viwili toafuti
Umri umemtupa Mkono miaka 79 sio haba, maana umri wa kuishi kwa Mujibu wa Biblia ni miaka 70 kwahiyo ukivuka huo umri ni neema tu
 
Dotto anatamba anga za maziwa makuu. Hapo kagame Anazo furaha zote Kwa kuwa ndugu yake dotto mashaka Biteko ni naibu waziri mkuu, na Kulwa masunga Biteko akitarajia kuwa mbunge wa busanda 2025. Masunga Kwa kisukuma ni maziwa fresh

pk ndo big boss wa tanzagiza …
 
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni amekutana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko Ikulu ya Entebbe nchini humo ili kupokea salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru wa Nchi ya Uganda.

Mhe. Rais Museveni ameishukuru Serikali ya Tanzania na kuongeza kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa na mafanikio makubwa ya kihistoria na kiuchumi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu alikabidhi zawadi kwa Mhe. Rais Museveni kama njia ya kuthamini mchango na ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stephen Byabato, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe Balozi Stephen Mbundi pamoja na viongozi wengine kutoka ubalozi wa Tanzania nchini Uganda.
Huyu mama gauni duh
 
Back
Top Bottom