Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nitaomba muniwie radhi pale nitaposema mengine sio lazima ya kuhitaji fedha ila ni ubunifu wa ile familia tu. Mfano hiyo picha ya juu fito za nyumba zinaonekana kabisa, jee udongo unauzwa? Na kama kazi ni nyingi basi hata baada ya mavuno haiwezekani angalau kukandika kwa udongo na kuunyoshea (plaster) hata kwa udongo wenyewe lakini nyumba ikaonekana nadhifu?
Na hiyo picha inayoonyesha uwepo wa takataka tunasubiri Manispaa waje kuzoa wakati anaeishi hapo ndiye anayeugua malaria na maradhi mengine yanayotokana na kuwepo kwa nzi?
Sio kwamba namdharau mtu na namwomba Mwenyezi Mungu anisamehe kama nimekufuru!