Rais wa Young Africans Eng. Hersi "Fainali ya CAF Champions League msimu huu ni baina ya Al Ahly dhidi ya Mamelodi Sundowns"

Rais wa Young Africans Eng. Hersi "Fainali ya CAF Champions League msimu huu ni baina ya Al Ahly dhidi ya Mamelodi Sundowns"

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
MICHEZO Rais wa klabu ya Yanga SC akiwa katika mahojiano na Televisheni ya Al Ahly amesema "binafsi naamini fainali ya CAF Champions League msimu huu ni baina ya Al Ahly dhidi ya Mamelodi Sundowns”, Al Ahly na Mamelodi ni timu zenye mikakati na ubora wa hali ya juu kwasasa Barani Afrika.

Hersi aliendelea kusisitiza, “ikumbukwe Al Ahly ndio timu yenye uwekezaji mkubwa sana tena inapofika hatua za mtoano katika michuano hii, huku Mamelodi wakiwa ni mabingwa AFL na sidhani itakuwa rahisi kwao kuishia robo au nusu fainali.

Maneno ya Rais wa Yanga, Eng. Hersi Ally Said kupitia mahojiano na Televisheni ya Al Ahly. #EastAfricaTV
 
Maneno yenye adabu na utii uliotukuka. Sio kelele kelele za kijinga.
 
Mamelodi kwanza hao wengine wagombee hio nafasi moja
 
Msemakweli Ni Mpenzi Wa Mungu
Nasema Uongo Ndugu Zangu?
Al Ahaly vs Mamelod
 
Amed ally anasema hata vilabu vyote duniani viungane ili vichene na Thimba jumamosi n lazma wafungwe eeeti
 
Kwamba Utozidadi hawana uwezo wa kwenda fainali?
 
Zile sauti za vyura zimeanza kupungua makali baada ya kupewa Mamelodi.
 
Back
Top Bottom