Rais wa zamani Ufaransa kufikishwa Mahakamani kwa tuhuma za ufisadi

Rais wa zamani Ufaransa kufikishwa Mahakamani kwa tuhuma za ufisadi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy atafika mahakamani Jumatatu ambapo anatuhumiwa kujaribu kutoa hongo kwa jaji na kupelekea ushawishi, ikiwa ni moja ya uchunguzi kadhaa wa jinai ambao unatishia kuweka aibu kubwa katika utumishi wake wa muda mrefu wa kisiasa.

Waendesha mashtaka wanadai Sarkozy alijitolea kumpatia kazi ya fedha nyingi Jaji Gilbert Azibert huko Monaco kwa malipo ya habari ya siri juu ya uchunguzi wa madai kwamba Sarkozy alikuwa amekubali kupokea malipo haramu kutoka kwa mrithi wa L'Oreal Liliane Bettencourt kwenye kampeni yake ya urais ya mwaka 2007.

Sarkozy, ambaye aliongoza Ufaransa kutoka mwaka 2007 hadi 2012 na amebaki na ushawishi mkubwa kati ya wahafidhina, amekanusha makosa yoyote katika uchunguzi wote dhidi yake na kupambana vikali ili kesi hizo zifutwe.

Wachunguzi kutoka mwaka 2013 walikuwa wakisikiliza mazungumzo kati ya Sarkozy na wakili wake Thierry Herzog walipokuwa wakichunguza madai ya ufadhili wa Libya katika kampeni ya Sarkozy ya mwaka 2007.

Wakati wakichunguza waligundua kwamba Sarkozy na wakili wake walikuwa wakiwasiliana kwa kutumia simu za mkononi zilizosajiliwa kwa majina ya uwongo. Simu ya Sarkozy ilisajiliwa kwa jina la Paul Bismuth.
 
MUNGU mkubwa sana,,laana ya Gaddafi imeanza kujibu sasa..

Huyu rais wa ufaransa ndy aliyemuua Gaddafi..
Yeye ndy aliyeongoza genge la wahuni kuvamia Libya..
Inasemekana alikuwa partner mkubwa sana wa Gaddafi..
Ikafikia kipindi alikopa millions of euros kwa Gaddafi kwa makubaliano maalum kuendesha kampeni za uchaguzi..

Aliposhinda uchaguzi akaja kumgeuka Gaddafi baada ya kudaiwa kurudisha pesa zile na Gaddafi..

Akatengeza zengwe na wahuni wenzie wa EU na marekani kwa faida yake..

At least Obama alikiri hadharani kwamba ,,
we were wrong to kill Gaddafi..

Huyo ni wa kufunga kabisa..
 
Huyu Sarkozy aliongoza kampeni ya kumng'oa Marehemu Ghadafi wakati Ghadafi alifadhili kampeni zake za kisiasa.

Alifanya hayo akijua kifo cha Ghadafi kingepoteza ushahidi kwa ufadhili huo na tuhuma zingine za rushwa, Sasa anavuna alichopanda.
 
Sarkozy, Blair na Bush walifanya kazi nzuri sana. Hawakutoa nafasi kwa madikteta na magaidi kujimwambafai. Kama binadamu kuna kokosea au at times kupewa taarifa za uongo na kuzifanyia kazi.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom