Pre GE2025 Rais, wabunge na madiwani wote waliobebwa na Magufuli waanze sasa kuaga, 2025 hakuna atakayetoboa!

Pre GE2025 Rais, wabunge na madiwani wote waliobebwa na Magufuli waanze sasa kuaga, 2025 hakuna atakayetoboa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Hakuna siri tena, hali huko mitaani imeshakuwa tete, raia wameanza kusanda, wameanza kufunguka na kuweka wazi kuwakataa wazi wazi viongozi wote waliobebwa na Magufuli mwaka 2020.

Viongozi wote waliobebwa na Magufuli wapo katika makundi matatu. Kundi la kwanza ni wale ambao walipitishwa kinguvu na kihuni kwa kutangazwa ni washindi wa uchaguzi wakati wapiga kura hawakuwapigia kura au kuwataka. Hapa inajumuisha waliopitishwa bila kupingwa, waliokataliwa kwa kura lakini wakapitishwa kinguvu ikijumuisha na lile kundi la Covid 19.

Kundi la pili ni wale waliopita kwa upepo wa kisiasa wa Magufuli tu. Bila Magufuli wasingejulikana na wala wasingepita popote kisiasa ikiwemo ndani ya CCM.

Kundi la tatu ni kundi la viongozi waandamizi ambao walikuwa ni timu ya utawala wa Rais Magufuli, hili likijumuisha na Rais wa sasa (mama Samia). Wapo wengine katika mazingira ya sasa ya kisiasa ndani ya CCM huenda wasitoboe (mfano ni Nape, January).

Katika mazingira ambayo hata mwenyekiti wa CCM taifa (Rais Samia Suluhu) hana uhakika wa moja kwa moja wa kutoboa kwenye uchaguzi mkuu wa 2025 kwa sababu ya kuchokwa au kutokuaminiwa kabisa na watanzania wengi (kwa sababu za udhaifu wa kusimamia uwajibikaji serikalini, ulanguzi wa rasimali za taifa, ujinsia, uzanzibar na ushawishi duni kisiasa), hakuna tena mtu wa kumbeba mwenzake.

Safari hii huenda kikawaka, kila mwanaCCM ajipange kubeba mzigo wake mwenyewe.
 
Itakuwa mchuano kati ya asilia na wa kuja
 
Awamu hii aina mwamko wa vijana kupiga kura usitegee hayo unayowaza lolote linaweza tokea
 
Kumbuka kila mbunge anaondoka na 250m/= kama kiinua mgongo! Hizo hizo wakitumia ujinga wetu watatoboa mchana kweupe!
Sema safari hii kwenye kura za maoni za kupitisha wagombea kwenye ubunge na udiwani ndiyo watatoana roho! Bila hivyo wanajua wapiga kura wanahitaji nini! Wanataka kofia,vitenge,mashati ya kijani! Ni kipindi watakuja na ahadi za kusomesha watoto,ni kipindi ambacho watagawa mitungi ya pombe bure hasa kule vijijini,ni kipindi ambacho watalisha pilau bure watu,ni kipindi watakachohudhuria msiba na arusi na kutoa matamko ya Mama kafanya tuchagueni,na kila aina ya mbwembe! Na watu watapiga makofi ikifika kwenye sanduku la kura Chama pendwa!
 
Back
Top Bottom