Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Kivyovyote vile utakavyo muona kwa suru au kumsikiliza kwa maskio anachosema matokeo au hitimisho lake kwako, ni kwamba utamuamini na utampenda tu, ndivyo alivyo.
Na hiyo ni Neema, Baraka na karama ya kipekee sana aliyojaliwa na Mungu. Hana hofu, kiburi, ubishi, majivuno wala ubinafsi kuwajumuisha watu tofauti tofauti kwenye serikali yake.
Ana hekima na busara ya hali ya juu sana, anajua siasa, hana papara, anafahamu kuongoza watu na amejipanga na kujiandaa kupita kwenye changamoto zenye moto, joto au baridi la kisiasa kwa ujasiri na uhakika wa kufaulu mitihani yote bila mbambamba yoyote.
Ni mwanasiasa msikivu, mtulivu, kiongozi na mtawala mwenye utaratibu sana. kwenye machafuko anahimiza amani na utangamano. kwenye chuki anahubiri furaha. kwenye giza anapeleka nuru. Kwenye migawanyiko anazidisha juhudi za kuwaletea watu pamoja, kwa wanyonge na waliokata tamaa anawapa matumaini na ujasiri wa uhakika wa maisha yao.
Ni mtu wa kusema na kutenda. Ni msikivu msomi makini, hodari wa kuahidi na kutimiza ahadi zake kwa wakati kwa wananchi aliyo waahidi.
Ni suala la muda tu anakuja na Baraza la mawaziri jumuishi, litakalowaunganisha wakenya, litakalo konga nyoyo za wakenya wa makundi mbalimbali, na lisilo na sura ya ukabila, udini au ukanda, bali litakalo zingatia maslahi mapana ya Wakenya wote.
Gen z wametulia, Kenya imetulia, wakenya wamefaulu mitihani wa amani kwa pamoja.
Mungu Mbariki Rais Dr. Wiliam Arap Ruto,
Mungu ibariki Jamuhuri ya watu wa Kenya 🐒