Rais Xi asema malengo yao na Urusi ni mamoja

Rais Xi asema malengo yao na Urusi ni mamoja

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Wakati mpango wa ziara ya raisi wa china ndugu XI ulipowekwa wazi viongozi wa Ukraine na Marekani walimuomba kiongozi huyo akifika Urusi amsisitize raisi Putin kusitisha vita ambavyo vimeshavuka mwaka mpaka sasa.

Kwa bahati mbaya Xi alipofika huko alikuwa na mazungumzo ya kuimarisha umoja baina yao na katika hitimisho akaweka wazi kuwa malengo ya China na Urusi ni ya aina moja .Katikati ya mazungumzo yao waliitana marafiki wakubwa na Xi akawaomba warusi wamchague tena Putin pindi utakapokuja uchaguzi mwengine.

Ziara ya Xi nchini Urusi imefuatiwa na ziara ya waziri mkuu wa Japan bw.Kishida ambaye ameitembelea Ukraine kwa kushtukiza. Bado lengo la ziara ya Kishida huko Kyiv halijawekwa wazi.

2023-03-20T144602Z_1887968151_RC2QXZ9JIBKI_RTRMADP_3_CHINA-RUSSIA-DIPLOMACY-XI-PUTIN.jpg
 
Back
Top Bottom