SI KWELI Rais Yoweri Museveni amelazwa ICU

SI KWELI Rais Yoweri Museveni amelazwa ICU

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Salaam Ndugu zangu,

Nimekutana na taarifa kutokea twitter zikidai kwamba Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amelazwa kwenye chumba cha uangalizi maalumu.

Je, kuna ukweli wa taarifa hii?

1686554270592.png

 
Tunachokijua
Tangu Juni 8, 2023 kumeibuka tetesi zinazodai kwamba Rais wa Uganda Yoweri Museveni amelezwa na yupo kwenye chumba maalumu cha Wagonjwa mahututi (ICU). Taarifa hiyo ilisambaa kwenye kurasa mbalimbali za mitandao ya hasa twitter kama ifuatavyo:

Ukurasa wa Twitter usio rasmi unaojiita Citizen TV Kenya siku ya Juni 8, 2023 uliandika "Rais wa Uganda, Kaguta Museveni amepelekwa ICU kutokana na afya yake kudhoofika. Mwanawe, Jenerali Muhoozi, ameitisha mkutano wa familia."

Tetesi zilizoibuliwa na chanzo hicho zilinukuliwa na kurasa nyingine kuanza kusambaa mpaka kwenye mitandao mingine ya kijamii. Watu wengi mitandaoni walishtushwa na habari hiyo huku baadhi ya maoni yalihusisha taarifa hiyo na Suala la Museveni kusaini muswada kupinga mapenzi ya jinsia moja hivi karibuni huku wengine wakipinga wakieleza kuwa ni uzushi.

Je, tetesi hizo zimesababishwa na nini?
JamiiForums imechunguza ili kujua chanzo cha tetesi ambapo imebaini kuwa tetesi hizi ziliibuka kutokana na taarifa iliyotoka siku ya Juni 8, 2023 ambayo ilieleza kwamba Rais Yoweri Museveni amepata mafua makali yanayohisiwa kuwa ni Covid-19. Taarifa ya kuumwa kwa Museveni ilithibitishwa na Wizara ya Afya ya Uganda.

Je, Rais Yoweri Museveni amelazwa ICU?
JamiiForums imebaini kuwa chanzo kilichotoa taarifa hiyo si rasmi na kinatumia jina linalofanana na Chombo cha Habari nchini Kenya

Zaidi ya hayo, JamiiForums imepitia vyanzo mbalimbali vya habari vya kuaminika vya nchini Uganda lakini hakuna chanzo kilichoripoti Museveni kuumwa kiasi cha kupelekwa chumba cha Wagonjwa mahututi (ICU).

Zaidi ya hayo, Mnamo Juni 9, 2023 Rais Museveni kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter alitoa taarifa kuwa yupo salama na alikuwa katika siku ya tatu tangu apatwe na Covid-19 na anaendelea vizuri. Sehemu ya taarifa hiyo ilieleza:

"Sasa ni siku ya 3 tangu nipatwe na Corona. Jana, katika siku ya 2 nilihisi usingizi sana muda wa saa tano asubuhi. Nilipoamka, nilikuwa mwenye nguvu na nilimuandikia hotuba fupi kwa Mheshimiwa Nabbanja Luwero leo. Nilimtuma Nabbanja Luwero kwa sababu Makamu wa Rais, Alupo, alienda kutuwakilisha kwenye mkutano wa Lusaka- COMESA."
Pia, mnamo Juni 11, 2023 Rais Museveni alitoa taarifa ya kuendelea vizuri katika ukurasa wake wa Twitter. Sehemu ya taarifa hizo ilieleeleza:
"Sasa ni siku ya 5 tangu nipate corona. Jana usiku, nililala vizuri sana hadi saa kumi za usiku (ambazo Wazungu huita saa nne asubuhi). Wakati huu, nilikuwa sina maumivu ya kichwa yasiyo kali (dull headache), wala kupiga kidogo kidogo (enkuratima) juu ya kichwa (oruhoora-hoore)."

Sambamba na hilo, Juni 11, 2023 ukurasa rasmi wa Ikulu ya Uganda uliweka picha zikimuonesha Museveni akionekana mwenye afya njema na akiwa anaandika kitu kwenye makaratasi tazama hapo chini
Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo vilivyopitiwa na JamiiForums taarifa zilizoenea zikidai kuwa Rais Yoweri Museveni amelazwa kwenye chumba cha Wagonjwa mahututi zinakosa mashiko.

---
UPDATE
- Leo tarehe 14/06/2023 Rais Museven amejitokeza na kukanusha taarifa kwamba aliumwa na kulazwa chumba cha Wagonjwa Mahututi.

Aidha, Mkuu huyo wa nchi pia aliwalaumu baadhi ya wananchi kutoka nchi ya jirani ya Kenya kwa kusambaza uvumi kuhusu hali ya afya yake. Katika kufafanua jambo hilo Museven Amesema:
"Niliona watu wachache nafikiri ni kutoka Kenya wakisema niko ICU (Chuma cha wagonjwa mahututi) sasa kama ningekuwa ICU serikali ingeijulisha nchi, kwani kuna nini cha kuficha,”amesema Museveni."
Kuna habari nimesikia leo imenipa kidogo maswali mengi
Kuwa rais wa uganda Yupo mautiuti
Je ni za Kweli ?
Kama ni Kweli USA [emoji112][emoji112][emoji850][emoji24] ndo mambo yenu Haya
 
Kuna habari nimesikia leo imenipa kidogo maswali mengi
Kuwa rais wa uganda Yupo mautiuti
Je ni za Kweli ?
Kama ni Kweli USA [emoji112][emoji112][emoji850][emoji24] ndo mambo yenu Haya
yes ila ni kiwimbi kidogo cha crona kimempitia,not serious... All in all, kufa na umri wake huwezi kuvitenganisha sana...
 
Back
Top Bottom