Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Polisi wa Uganda wameshtumiwa kwa ukatiliImage caption: Polisi wa Uganda wameshtumiwa kwa ukatili.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameshutumu kile alichokitaja kuwa utovu wa nidhamu unaotekelezwa na vikosi vya usalama vinavyowatesa au kuwapiga raia wa Uganda wa kawaida.
Bwana Museveni ameongeza kuwa vikosi vya usalama vinavyowatesa washukiwa ni wavivu na hawataki kufanya uchunguzi stahiki na kukusanya ushahidi wa kutosha unaohitajika.
Wakati wa hotuba yake ya kitaifa iliyopeperushwa kupitia televisheni, picha za video za washukiwa waliokamatwa kwa kumpiga risasi Waziri wa Ujenzi Jenerali Katumba Wamala, ambao wanadaiwa kuteswa wakiwa kizuizini, zilichezwa.
Rais alisema ukatili "utaharibu uhalali wetu" na kuongeza kuwa "hakuna mtu anayepaswa kumpiga raia yeyote wa Uganda. Matumizi ya "mateso" sio lazima na ni makosa".
"Kwanini umpige mtu? Kwasababu wewe ni mvivu sana wa kuwahoji. Ni wahalifu lakini mateso ni makosa", rais alisema.
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi ambaye pia anajulikana kama Bobi Wine amemshutumu rais kwa kutokuwa mkweli katika matamshi yake juu ya ukatili unaotekelezwa na polisi.
"Ninaweza kufikiria jinsi waathiriwa waliofanyiwa unyama chini ya uongozi wake wanavyohisi wakati wanamwona bila aibu yoyote akizungumza uongo, bila kujali kabisa matatizo yao.
Kwa nyinyi nyote wahanga wa mateso, muliowekwa kizuizini kinyume cha sheria na waliotekwa nyara, ninaweza kuhakikishia kwamba kutakuwa na siku haki itatendeka", Bw. Kyagulanyi amenukuliwa na tovuti ya habari ya Nile Post akisema.
Bwana Kyagulanyi amekuwa mwathirika wa ukatili unaotekelezwa na polisi mara kadhaa.
Mnamo mwezi Januari, shirika la Human Rights Watch lililitoa wito kwa vikosi vya usalama vya Uganda kukomesha tabia ya matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya raia wakati nchi hiyo ikijiandaa kufanya uchaguzi ambao ulighubikwa na vurugu na vitisho dhidi ya wapinzani.