Nchi yetu haiishiwi vituko. Rais yuko Marekani anatibiwa, Rais mtarajiwa Lowassa ambaye anaongoza kwenye kura za maoni naye yuko matibabuni Ujerumani. Walau tunajua Rais anaumwa tezi dume, anachoumwa Rais mtarajiwa hatukijui. Walau Rais anaumwa mwishoni mwa utawala wake lakini Rais mtarajiwa anaumwa hata hajaanza kampeni na amekuwa akienda Ujerumani mara kwa mara. Hii imekaaje wakuu? Si wakati sasa wa kutaka wagombea urais wachunguzwe afya zao na kuthibitishwa na bodi ya madaktari bingwa kabla hawajapitishwa na vyama vyao?